Whozu, Billnass na Mbosso wapunguziwa adhabu na BASATA

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapunguzia adhabu wasanii wa bongofleva nchini Tanzania, Whozu, Billnass na Mbosso na kuwataka wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi...

0

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewapunguzia adhabu wasanii wa bongofleva nchini Tanzania, Whozu, Billnass na Mbosso na kuwataka wasanii hao kulipa faini ili waweze kuruhusiwa kufanya kazi za sanaa.

Uamuzi huo umetolewa leo katika kikao cha kusikiliza rufaa ya wanamuziki hao ambao BASATA iliwafungia kufanya kazi za Sanaa kwa miezi sita kwa msanii Whozu na miezi mitatu kwa msanii Billnass na Mbosso pamoja kulipa faini ya TZS milioni tatu kila mmoja kwa kutoa video ya wimbo wa ‘Ameyatimba’ ambao ulikwenda kinyume na maadili ya Kitanzania.

Maamuzi hayo yamefikiwa kwenye kikao chini ya uongozi wa Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro kilichofanyika uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es salaam ambapo msanii Whozu amepewa masaa sita ili kutekeleza azimio la kushusha wimbo huo kwenye “digital platforms” zote kwa mujibu wa makubaliano.

Aidha, Waziri Ndumbaro amewahasa wasanii hao na wengine nchini kutumia ubunifu kwa kufuata taratibu ulioainishwa katika mwongozo wa uzingatiaji maadili katika kazi za sanaa.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted