Miaka mitatu ya Urais wa Samia akiwa mwanamke wa kwanza Tanzania kushika wadhfa huo.

Rais Samia Suluhu Hassan alishika  hatamu ya nchi kufuatia kifo cha mtangulizi wake huyo hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo tangu lipate uhuru.

0

Tarehe kama ya leo mwaka 2021, Samia Suluhu Hassan aliyekuwa Makamu wa Rais wa Tanzania wakati huo aliapishwa kuwa Rais, kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano Hayati John Pombe Magufuli ambaye alifariki akiwa madarakani.

Rais Samia Suluhu Hassan alishika  hatamu ya nchi kufuatia kifo cha mtangulizi wake huyo hivyo kuwa mwanamke wa kwanza kuongoza taifa hilo tangu lipate uhuru.

Aliapishwa, katikati ya kipindi cha janga la corona, mwezi Machi 19,2021 baada ya mtangulizi wake John Magufuli alipofariki ghafla alipokuwa madarakani. Na mara tu aliposhika uongozi , alinukuliwa akisema kuwa ‘‘yeye na Magufuli walikuwa kitu kimoja.’’

Lakini hatua zake Katika muda wa uongozi wake imedhihirisha mambo tofauti.

Katika siku yake ya kwanza madarakani kama Rais wa Tanzania Rais Samia, alinukuliwa akisema alikutana na orodha ya masuala ambayo yalielezwa na wasaidizi wake kama “miiba” kwenye utawala wake.

Mojawapo lilikuwa ni mgawanyiko uliopo baina ya Watanzania kutokana na tofauti za kisiasa zilizotokana na miaka mitano ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli.

Kutokana na hayo aliamua kuja na falsafa ya 4R kama mfumo wake wa uongozi ambapo aliamini kwamba italeta amani na mshikamano wa taifa.

Falsafa hiyo alisema itatumika zaidi katika kipindi cha uchaguzi kwa kile alichodai kwamba ili nchi iweze kupiga hatua kubwa kimaendeleo ni lazima iendelee kuwa moja kwa kuishi kwa umoja na suala la uchaguzi litazingatia hilo.

4R ni kifupisho cha maneno ya Kiingereza Reconciliation (Maridhiano), Resilience (Ustahimilivu), Reform (Mabadiliko) na Rebuiding (Kujenga upya). 

Falsafa hii ndiyo anayoitumia sasa, anatajwa kama rais aliyeiokoa nchi katika udiktekta wa siasa ambao ulifanywa na mtangulizi wake, lakini pia ndani ya miaka mitatu ya uongozi wa Samia ametajwa kama kiongozi aliyeboresha miuondombinu ya kijamii kwa sehemu kubwa.

Hata hivyo anakosolewa vikali na wakosoaji wakiwemo wanaharakati kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo na kumuweka wazi kwamba hana tofauti na mtangulizi wake hayati Magufuli kutokana na yanayoendelea ikiwemo ya uvunjifu wa Katiba.

Leo anatimiza miaka mitatu tangu apokee kijiti cha uongozi kikatiba kama Rais wa nchi.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted