Mtoto Mwenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) Ajeruhiwa Kwa Panga Geita

Kamanda Jongo alisema kuwa majera ya mtoto na silaha iliyokutwa eneo la tukio ni wazi aliyafanya tukio hilo hakuwa na lengo la kuondoka na kiungo chochote.

0

Na Mariam John

Mtoto wa miaka 10 mwenye ulemavu wa ngozi mkazi wa mtaa wa mtakuja Kata ya Katoro wilayani Geita amejeruhiwa kwa panga na mtu asiyejulikana na kuzua taharuki.

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita kamishna Safia Jongo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo kwa uchunguzi wa awali unaonesha kuwa tukio hilo ni la kupangwa.

Kamanda Jongo alisema kuwa majera ya mtoto na silaha iliyokutwa eneo la tukio ni wazi aliyafanya tukio hilo hakuwa na lengo la kuondoka na kiungo chochote.

Mganga mfawidhi wa hospital ya mji wa Geita Thomas Mafuru amethibitisha kumpokea mtoto huyo ambae alikuwa amejeruhiwa kichwani na mkononi nakwamba anaendelea vizuri.

Kwa upande wake mama mzazi wa mtoto huyo na mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo wamesema wamelipatwa na hofu juu ya tukio hilo.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted