Wafanyakazi wa Kenya Airways waliozuiwa DRC waachiliwa

Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Kenya Airways waliokuwa wamekamatwa katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo wameachiliwa huru, afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje nchini Kenya...

0

Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Kenya Airways waliokuwa wamekamatwa katika nchi ya Kidemokrasia ya Congo wameachiliwa huru, afisa mwandamizi kutoka wizara ya mambo ya nje nchini Kenya amesema.

Afisa mkuu mtendaji wa Shirika hilo Allan Kilavuka, Kenya Airways itarejelea safari zake za kuelekea Kinshasa,

Kitengo cha ujasusi wa kijeshi cha Congo kiliwazuilia wafanyakazi wawili wa shirika hilo la ndege mnamo Aprili 19, kwa madai ya kukosa nyaraka za forodha kwenye baadhi ya mizigo ya thamani.

Kampuni hiyo ilisema haikumiliki shehena hiyo kwa sababu karatasi za msafirishaji hazikuwa zimekamilika na kuelezea kukamatwa kwao kama “kinyume cha sheria” na kusimamisha safari za ndege kuelekea mji mkuu wa DRC siku iliyofuata.

Wawili hao walizuiliwa licha ya agizo la mahakama kutaka waachiliwe.

Mmoja wa wafanyikazi alikuwa Mkenya, mwingine raia wa Congo

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted