Kamanda wa kundi la ADF akamatwa na Jeshi la Uganda

Watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa katika operesheni ya kumsaka kamanda huyo. Watu hao walipatikana mkoani Ituri Mashariki mwa DRC. Bidhaa za kutengenezea mabomu pia zilipatikana huko katika harakati...

0
Photo courtesy

Kamanda wa kundi la waasi la ADF linaloshirikiana na kundi la dola la kiislamu, ambaye ni mtaalamu wa kutengeneza mabomu yaliyotumiwa na kundi hilo kutekeleza mashambulizi mabaya, ameweza kukamatwa na Jeshi la Uganda.

Wakidhibitisha kukamatwa kwake, Wanajeshi wa Uganda walisema kuwa Kamanda huyo Anywari Al Iraq ambaye ni raia wa Uganda, alikamatwa katika maeneo ya jangwani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kunakopatikana kundi la waasi la ADF.

Photo courtesy

Watu tisa wakiwemo watoto waliokolewa katika operesheni ya kumsaka kamanda huyo. Watu hao walipatikana mkoani Ituri Mashariki mwa DRC. Bidhaa za kutengenezea mabomu pia zilipatikana huko katika harakati ya kufanya msako huo.

Kundi hilo la waasi wa ADF limekuwa na ngome yake Congo, licha ya kuwa uasi wake umekuwa ukitekelezwa nchini uganda.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted