Klabu ya Simba yamtimua Robertinho
Klabu ya Simba SC imeachana na kocha wao Robert Oliveira ‘Robertinho’ baada ya makubaliano ya pande zote mbili kwa maana ya klabu na mhusika.
Klabu ya Simba SC imeachana na kocha wao Robert Oliveira ‘Robertinho’ baada ya makubaliano ya pande zote mbili kwa maana ya klabu na mhusika.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Dkt. Francis Michael, ametoa muda wa siku tatu kwa Afisa elimu Mkoa wa Songwe kwa kushirikiana na taasisi nyingine ikiwemo Jeshi la Polisi kuwasaka watu wote waliohusika kuwakatisha masomo wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na kueleza hatua zilizochukuliwa kisha apewe taarifa.
Mkutano huo unalenga kujadili juhudi za SADC katika kuimarisha hali ya amani, ulinzi na usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kufuatia mapigano ya muda mrefu yanayoendelea nchini humo yakitekelezwa na vikundi vyenye silaha katika majimbo ya Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri.
Huo ni utafiti wa saba katika mfululizo wa utafiti wa kitaifa wa kidemografia na afya uliowahi kufanyika Tanzania mwaka 1991/92 ambapo kwa mujibu wa matokeo ya utafiti huo, taarifa za ujauzito kwa wanawake wenye umri wa miaka 15 hadi 49 kwa kipindi cha miaka mitatu kabla ya utafiti huo, zimeonesha asilimia 90 walizaa watoto hai na asilimia 10 walipoteza ujauzito.
Makonda amewasili akiwa kwenye bodaboda kwa kile kilichodaiwa kuwa alishindwa kufika na gari lake kutokana na msongamano wa magari na umati wa watu uliojitokeza kwenye eneo la ofisi hiyo
Mwabukusi ameeleza masikitiko yake kwa Serikali kusaini mkataba na DPW ya Dubai katika uendelezaji wa bandari ya Dar es Salaam akidai kuwa bado mapungufu hayajaondolewa na hata kipindi cha miaka 30 ya mkataba huo ni kirefu ikilinganishwa na raslimali inayoenda kuwekezwa.
Shilingi imekuwa ikishuka kwa miaka kadhaa na kuporomoka kwa karibu asilimia 24 katika mwaka uliopita, chini ya shinikizo la viwango vya juu vya deni na kupungua kwa mapato ya serikali.
Kampuni kubwa ya usafirishaji ya Dubai DP World ilitia saini mikataba mitatu siku ya Jumapili na serikali ya Tanzania ya kuendesha sehemu ya bandari ya Dar es Salaam kwa miaka 30 chini ya mkataba wenye utata unaohusu bandari zote za nchi.
Wanawake wanne wamefariki dunia katika mkanyagano magharibi mwa Kenya leo Ijumaa baada ya umati wa watu kuogopa mlio uliotokana na kumwagika kwa chai ya muuzaji mmoja kwenye moto wakidhanini ni gesi ya kutoa machozi .
Kituo cha daladala cha Kivukoni jijini Dar es Salaam kitafungwa kuanzia kesho Oktoba 21 kupisha upanuzi wa kituo cha mabasi yaendayo haraka cha Kivukoni awamu ya kwanza.