visual-link-preview
domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init
action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6121Tamthilia ya \u2018\u2019Echoes of War\u2019\u2019 ya Shule ya Wasichana ya Butere, inazidi kuzua hisia mseto nchini Kenya hususan kuhusu uhuru na haki ya kusema na udhibiti wa serikali.<\/p>\n
<\/p>\n
Tamthilia hiyo, iliyoandikwa na aliyekuwa Seneta wa Kakamega Cleophas Malala, imezungumzia pakubwa madhila, mahangaiko na hali ngumu ya Maisha wanayopitia kizazi cha vijana alamarufu Gen Z. Pia inazungumizia utawala na haki za kijamii. Matukio haya yametoa taswira mbaya katika tasnia hiyo ya Michezo ya Kuigiza la Kitaifa inayofanyika jijini Nakuru.<\/p>\n
Mzozo ulianza Alhamisi wakati wanafunzi wa shule hiyo walikosa vifaa muhimu kwa ajili ya tamasha hiyo, ikiwa ni pamoja na mfumo wa vipaza sauti, vifaa vya kuigiza, ukosefu watazamaji, walimu wao na msimulizi kwa mchezo wa kuigiza bwana Malala. Wanafunzi hao walifika katika ukumbi wa kuigiza na badala yake kuimba wimbo wa taifa na kisha kuondoka ukumbini kwa ghadhabu. Walitoka nje kwa huzuni na kuanza kuimba nyimbo za kukashifu serikali.<\/p>\n Polisi walilazimika kutumia mabomu ya machozi dhidi ya wanafunzi hao waliokuwa wakifanya maandamano baada ya kuzuiwa kuonyesha onyesho lao la \u2018Echoes of War\u2019 ambalo limekuwa kivutio nchini, katika tamasha la sanaa la National Drama Festivals.<\/p>\n Tamthilia hii, inayozungumzia mustakabali wa taifa baada ya vita kwa uongozi wa vijana, imekuwa kivutio kikubwa, ikielezea hali ya kisiasa na kijamii kwa kutumia mitindo ya kisasa kama teknolojia na mitandao ya kijamii. Hata hivyo, imeshuhudia upinzani mkali kutoka kwa serikali, ikiwemo polisi kutumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya wanafunzi na wanahabari waliokuwa wakifuatilia tamasha hilo.<\/p>\n Malala, ambaye alikamatwa kwa madai ya kuingia shuleni kwa ajili ya kuangalia mazoezi ya tamthilia hiyo, alikamatwa na polisi lakini aliachiwa baadaye bila mashtaka yoyote. Baada ya kuachiliwa, Malala alielezea jinsi wasichana wa Shule ya Butere walivyoonyesha ujasiri mkubwa kwa kususia onyesho hilo, akisema kwamba walistahili pongezi kwa hatua yao ya kishujaa.<\/p>\n Mashirika ya haki za binadamu kama Kamati ya Haki za Binadamu ya Kenya (KHRC) na Amnesty International pia yamekosoa vikali vitendo vya serikali, na kudai kuwa ni uvunjaji wa haki ya kisanii na uhuru wa kujieleza. Viongozi wa kisiasa kama Kalonzo Musyoka na Eugene Wamalwa wameungana na mashirika hayo, wakisema kuwa hatua za serikali ni za kiunyanyasaji na zinadhoofisha uhuru wa sanaa nchini Kenya.<\/p>\n Tamthilia ya Echoes of War imezua mjadala mkubwa kuhusu haki ya vijana katika kuchangia mazungumzo ya kisiasa, huku serikali ikikabiliana na upinzani kutoka kwa wataalamu wa sanaa na wananchi kwa jumla.<\/p>\n