Rais Biden awasili Angola kwa ziara ya siku tatu
Rais Joe Biden aliwasili Angola siku ya Jumatatu kwa ziara yake ya kwanza ya rais iliyosubiriwa kwa muda mrefu katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na atatumia safari hiyo ya siku tatu kukabiliana na ushawishi wa China kwa kuangazia mradi kabambe wa reli unaoungwa mkono na Marekani.