GST: Hakuna madhara yaliyoripotiwa kutokana na tetemeko la ardhi Dodoma.
Akizungumza leo na waandishi wa habari Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Gabriel Mbogoni alisema kuwa Februari 16, mwaka huu saa 12.13 jioni tetemeko lenye ukubwa wa Richert 4.9 lilitokea katika eneo la Makuru, Tarehe 17 Februari, saa 1:45 asubuhi tetemeko lenye ukubwa wa richer 4.3 lilitokea eneo la Makuru na Feburari 17, mwaka huu tetemeko lenye ukubwa wa richer 4.9 lilitokea katika eneo la Zuboro.