Chadema kuandamana kudai upatikanaji wa waliotekwa Tanzania
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema kuwa hadi Septemba 21, 2024, wana matarajio ya kuona hatua za dhati kutoka kwa Serikali, vinginevyo maandamano yatafanyika kama ilivyopangwa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, amesema kuwa hadi Septemba 21, 2024, wana matarajio ya kuona hatua za dhati kutoka kwa Serikali, vinginevyo maandamano yatafanyika kama ilivyopangwa.
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimesikitishwa na kulaani kitendo cha utekaji na kuuawa kikatili kwa kada wa Chadema Ali Mohamed Kibao aliyefariki siku moja baada ya kuchukuliwa na watu waliojitambulisha kuwa ni askari polisi katika basi ya la kampuni ya Tashrif linalofanya safari zake za Dar es salaam kwenda Tanga.
Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania umeungana na raia wengine wa taifa hilo kushtumu mauaji ya mwanasiasa wa chama cha upinzani Chadema Ali Mohammed Kibao.
Leo, Septemba 9,2024 mwili wa Ali Kibao, kada maarufu wa chama cha Chadema ambaye alifariki baada ya kutekwa umezikwa huku umati mkubwa wa watu umejitokeza kushuhudia safari yake ya mwisho iliyojaa huzuni ya kutafakarisha
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), Freeman Mbowe ametangaza kumfikisha Mahakamani aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Nyasa na Mbunge wa zamani wa chama hicho ambaye sasa ni kada wa CCM mchungaji Peter Msigwa kutokana na kauli za kumdhalilisha anazozitoa dhidi yake.
Kesi ya afande anayedaiwa kuwatuma vijana kubaka kwa kikundi na kumwingilia kinyume na maumbile binti mkazi wa Yombo Dovya jijini Dar es salaam, Fatma Kigondo inakuja leo baada ya mahakama kutoa hati ya wito kwa mara nyingine Agosti 23 mwaka huu.
Mwanamichezo wa Uganda, Rebecca Cheptegei, amefariki nchini Kenya siku nne baada ya kuteketezwa kwa moto na mpenzi wake, taarifa kutoka kwa maafisa wa michezo wa Uganda zilisema leo Alhamisi.
Miaka saba imepita tangu Tundu Lissu, mwanasiasa na kiongozi wa upinzani nchini Tanzania, aliposhambuliwa kwa risasi mnamo tarehe 7 Septemba 2017. Tukio hili lilileta mshtuko mkubwa siyo tu kwa watanzania bali pia kwa jamii ya kimataifa. Tangu tukio hili kutokea, bado upelelezi wa kina haujafanyika na watuhumiwa hawajashikiliwa, hali inayoendelea kutoa maswali mengi kuhusu usalama wa viongozi wa upinzani na uongozi wa kisheria nchini Tanzania.
Chama Kikuu cha Upinzani nchini Tanzania chama cha Chadema, kimesema utekaji unaoendelea nchini humo kwa zaidi ya asilimia 60 unafanywa na Jeshi la Polisi kupitia kikosi kazi maalum kilichoandaliwa kwa kazi hiyo.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema), kimepinga amri ya Serikali iliyochapishwa kwenye Gazeti la Serikali namba 673 la tarehe 02 Agosti, 2024, ambapo kwa mujibu wa chapisho hilo imewaondoa wananchi wote wa Tarafa ya Ngorongoro kwenye ardhi yao kwa kufuta Kata, Vijiji na Vitongoji vyote vya Tarafa hiyo.