Sheria ya kupinga ushoga sasa ni rasmi nchini Uganda
Rais wa Uganda Yoweri Museveni leo amesaini Muswada wa Sheria wenye utata dhidi ya mashoga, ofisi yake na bunge la nchi hiyo zilisema, ikianzisha hatua kali dhidi ya ushoga ambazo zimetajwa kuwa miongoni mwa sheria kali zaidi duniani.