Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo siku ya Alhamisi ilizindua mnada wenye utata wa vitalu 30 vya mafuta na gesi, licha ya onyo kwamba uchimbaji katika misitu ya mvua na peatlands nchini humo unaweza kuwa janga la kimazingira.
Kati ya vitalu 27 vya mafuta vilivyowekwa kwa mnada katika mji mkuu Kinshasa, tisa viko katika msitu mkubwa wa bonde la kati na eneo la peatlands magharibi mwa nchi.
Mashirika ya mazingira kama vile Greenpeace yameonya kwamba mipango ya kuchimba visima katika bonde la kati inaweza kutoa kiasi kikubwa cha gesi ya kuzuia joto na kuongeza joto ulimwenguni.
Akifungua mnada huo siku ya Alhamisi, Rais wa Congo Felix Tshisekedi alisema kuwa kazi ya utafiti itafanywa ‘kwa kutumia njia za kisasa zaidi za kiteknolojia zinazolinda mazingira.”
Uchimbaji wowote utakuwa chini ya mpango ulioundwa ili kupunguza athari mbaya kwenye mifumo ikolojia, aliongeza.
Tshisekedi pia alisema kuwa uzalishaji wa mafuta na gesi utaruhusu DRC kupunguza utegemezi wake katika uchimbaji madini — kwa manufaa ya watu wa Congo.
Takriban robo tatu ya wakazi wa DRC wa watu milioni 90 wanaishi chini ya dola 1.9 kwa siku, kulingana na takwimu za Benki ya Dunia, licha ya hifadhi kubwa ya madini ya dhahabu nchini humo, shaba hadi kobalti.
Waziri wa Hydrocarbons wa Congo Didier Budimbu alisema Alhamisi serikali itatoa haki za leseni kwa vitalu vitatu vya gesi baada ya muda wa miezi mitatu, na baada ya kipindi cha miezi sita kwa vitalu 27 vya mafuta.
“Kampuni zilizochaguliwa zitaitwa kutia saini mikataba ya kugawana uzalishaji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,” alisema.
Waziri huyo aliongeza kuwa DRC ina uwezo wa kuzalisha mapipa bilioni 22 ya mafuta, pamoja na mita za ujazo bilioni 66 za gesi asilia.
Wanasayansi wametoa maonyo kadhaa kuhusu maeneo ya peatland ya DR Congo, ambayo yanajumuisha eneo lenye ukubwa wa Uingereza.
Katika eneo lote la bonde hilo, karibu tani bilioni 30 za kaboni huhifadhiwa, watafiti walikadiria katika utafiti wa Nature mwaka wa 2016. Idadi hiyo ni takribani sawa na miaka mitatu ya utoaji wa hewa chafu duniani.