Shughuli za upiga kura Kenya zimeanza alfajiri ya leo Jumanne huku wakenya takriban milioni 22 wakijitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Wakenya watakuwa wanawachagua nafasi sita za uongozi, ikiwa ni rais, magavana, maseneta, wawakilishi wa wanawake, wabunge sawa na wawakilishi wadi.
Mgombea wa urais wa tiketi ya Kenya kwanza William Ruto tayari ameshiriki zoezi hilo. Ruto alipiga kura saa 6:15 am katika kituo cha shule ya msingi ya Kosachei iliyoko nyumbani kwake eneo la Sugoi kaunti ya Uasin Gishu.
Ruto alifika katika kituo hicho akiandamana na mkewe Rachel Ruto na wawili hao wakafululiza hadi katika kituo hicho baada ya kutoa sala ambapo walitoa wito kwa wakenya kuzingatia amani wakati huu baada ya zoezi hilo.
Naibu huyo wa rais alifuata zote sita za upiga kura pamoja na mkewe na kuondoka katika kituo hicho mara baada ya kukamilisha.
Akihutubia wanahabari baada ya kupiga kura Ruto ameonyesha kuwa imani kuwa na imani kwamba taifa la Kenya itazingatia Amani na kuwataka wapiga kura kupiga kura kwa njia ya huru.
“Nahisi vizuri sana kwamba baada ya miezi ya kampeni na kuzungumza na wakenya, asubuhi ya leo ndio siku yenyewe na tumejitokea kupiga kura na tunataka kuwa na uchaguzi wa amani,” amesema Ruto.
“Zoezi la kuchagua kiongozi mwingine wa Kenya ubaendelea nataka kuomba wapiga kura kujitokeza kwa wingi na kikubwa zaidi kuzingatia amani. Ni matumaini yake wakenya watafanya uamuzi bora,”
Ruto vilevile ameimiza tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kusimamia zoezi hilo kwa umakini pasi na kushurutishwa na yeyote.
Naibu huyo aliandamana na viongozi wengine kutoka ukanda wa Bonde la Ufa akiwemo seneta wa Nandi Samson Cherargei.
Wakati huo huo mgombea mwenza wa Azimio la Umoja-One Kenya Martha Karua pia amepiga kura katika eneo bunge la Gichugu kaunti ya Kirinyaga.
Karua alipiga kura dakika chache baada ya saa 6am jumanne katika kituo cha shule ya msingi ya Mugumoini kabla ya kuwataka wakenya kujitokeza kwa wingi na kushirika katika zoezi hilo la kihistoria.