Aliyozungumzia William Ruto katika hotuba yake ya kwanza kama rais

Kiongozi huyo wa taifa alitoa taswira ambayo serikali yake  itatumia kusukuma mbele uongozi alioutaja kama wa kila mkenya.

0
Rais William Ruto baada ya kuapishwa.

Rais William Ruto ameanza kutekeleza baadhi ya ahadi alizotoa wakati wa kampeini yake kwa kuteuwa majaji sita wa mahakama waliokuwa wamekataliwa na mtangulizi zake, kufanya idara ya polisi kujisimamia katika masuala ya fedha na kutafuta suluhuu ya kupata mbolea ya bei nafuu kwa wakulima.

Katika hotuba yake ya kwanza kama rais watano wa Kenya, rais Ruto pia alihaidi kuwashirikisha wakenya katika kuamua hatma ya mtaala wa umilisi (Competency Based Curriculum) na kutoa hakikisho kuwa karibuni atazindua hazina ya mahustler ambayo ilikuwa chambo kuu kwa wafanyibiashara wadogo kumuunga mkono wakati wa kampeini ya kuingia ikulu.

Kiongozi huyo wa taifa alitoa taswira ambayo serikali yake  itatumia kusukuma mbele uongozi alioutaja kama wa kila mkenya. Sera ambayo anasema itakuwa kinyume na hapo awali ambapo huduma kwa ummma ulipeanwa  kwa misingi ya vyama vya kisiasa na kimaeneo.

Uhuru wa taasisi mbalimbali

Akisadiki kuwa ushindi wake kuwa rais wa tano wa Kenya ulifanikishwa na hatua ya tume huru ya uchaguzi na mipaka (IEBC), idara ya usalama na mahakama ya upeo kusimama kidete na kukataa katakata kubadili uamuzi wa wakenya, Rais Ruto amehaidi kuwa serikali yake itaheshimu na kuimarisha taasisi mbalimbali nchini Kenya.

“Utenda kazi wa asasi za usalama nchini, tume ya IEBC na idara ya mahakama ilikuwa imewekwa kwenye mizani. Kwa kiwango kikubwa taasisi hizi zimedhihirisha kuwa zinaweza kuwa huru katika kutekeleza majukumu yao. Sasa tunaweza kutarajia kufanya vyema kabisa katika siku za usoni, na ninahaidi kuwa serikali yangu itahakikisha uhuru wa taasisi hizi umezidishwa hata zaidi kabla ya uchaguzi mkuu ujao,” alisema rais Ruto.

Kupiga jeki idara ya mahakama

Kando na kuwateua majaji  sita wa mahakama, rais Ruto alisema serikali yake itaongeza mgao wa idara ya mahakama kwa shilingi bilioni 3 kwa miaka mitano ijayo.

“Raslimali hizi sitasaidia kuimarishautoaji wa haki kwa kuongeza idadi ya korti kutoka kwa idadi ya sasa ambayo ni 25 hadi 100. Pia tutashirikiana na idara hiyo ya mahakama kujenga mahakama za juu katika kaunti saba ambazo bado hazina mahakama ya juu ,” alisema kiongozi wa taifa.

Hatua hiyo rais anasema itapelekea mahakama  kuharakisha  kuskiza na kuamua kesi za ufisadi na kesi zingine.

Kubuni jopokazi la kushughulikia mtaala wa umilisi

Kuhusu mtaala wa umilisi, rais Ruto amehaidi kubuni na kufanyia mageuzi jopo kazi ambalo litazinduliwa hivi karibuni kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali watakaoamua hatma ya mtaala huo wa umilisi.

“Tunafahamu uoga ulioko miongoni mwa wazazi kuhusu mfumo huo kwa jannuari mwakani kwa mara ya kwanza kutakuwepo darasa mbili zitakazo kalia mtihani wa kitaifa. Ningependa kuwahakikishia kuwa kutapatikana suluu ya kudumu kufikia wakati huo,” alisema Ruto

Ajira kwa rais anayestaafu

Akitambua juhudi za mpinzani wake mkuu aliyekuwa mgombea wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga na mgombea mwenza wake Martha Karua, rais Ruto amesema rais mstaafu Uhuru Kenyatta ataendelea kuwa kinara wa mipango ya amani katika kanda.

“Katika mipango wa ukanda wa Afrika Mashariki, Ethiopia na eneo la maziwa makuu, nimemuuliza kakangu mkubwa rais anayeondoka Uhuru Kenyatta ambaye amekuwa na uhusiano mzuri katika eneo nzima na akakubali kuendelea kuwa mwenyekiti mazungumzo hayo kwa niaba ya serikali ya Kenya,” alitangaza Rais Ruto.

Mbole ya bei nafuu kwa wakulima wa majani chai

Rais pia alikuwa na habari njema kwa wakulima wa majani chai, akisema seritali yake itaingilia kati na kusambaza mbolea kwa wakulima hao kwa bei ya chini na wakati huohuo kuhaidi kuweka mikakati ya kutoa suluu kwa matatizo yao.

“Kuwalinda wakulima wa majani chai, tumeweka mipango ya na mamlaka ya kuimarisha majani chai nchini (KTDA) kuanza kusambaza mbolea kwa shilingi 3500,” aliongeza rais

Ruzuku kwa bei ya mafuta

Katika tatizo la mafuta, rais Ruto alisema walipa ushuru ugharamia shilingi bilioni 144 na shilingi bilioni 60 katika kipindi cha miezi minne. Iwapo hiyo itaendelea  mlipa ushuru atagharamika shilingi bilioni 280 sawa na bajeti ya miradi ya serikali ya kitaifa.

“Pamoja na hayo kulikuwepo jaribio la kutoa ruzuku kwa unga kuelekea uchaguzi wa mwaka huu, shughuli ambayo iligharimu serikali shilingi bilioni 7 katika kipindi cha mwezi mmoja bila faidi yeyote,” alimalizia rais Ruto.

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted