Serikali ya Nigeria imetangaza sera inayolenga kukuza ufundishaji wa wanafunzi wa shule za msingi katika lugha za kienyeji badala ya Kiingereza.
Waziri wa Elimu Adamu Adamu aliwaambia wanahabari Jumatano kwamba mfumo mpya unaojulikana kama Sera ya Kitaifa ya Lugha umeidhinishwa kutekelezwa.
Inaeleza kuwa mafundisho kwa miaka sita ya kwanza katika shule za msingi yatakuwa katika lugha ya mama.
Kiingereza ni lugha rasmi ya Nigeria na taasisi zote za mafunzo zinaitumia kama lugha ya kawaida ya kufundishia na kujifunzia.
Lakini lugha za kienyeji sasa zitachukua hatua kuu, huku waziri wa elimu akisema “wanafunzi hujifunza vizuri zaidi” wanapofundishwa kwa lugha yao ya asili.
Alikubali kwamba kutekeleza sera hiyo mpya itakuwa changamoto kwa sababu “itahitaji kazi nyingi kuandaa nyenzo za kufundishia na kupata walimu”.
Changamoto nyingine ni idadi ya lugha zinazozungumzwa nchini Nigeria ni zaidi ya 600.
Haijabainika mara moja ni lini serikali itaanza kutekeleza mfumo huo mpya.
Mamlaka ya Nigeria inapendekeza kwanza kutoa vifaa vya kufundishia na walimu kwa lugha za wenyeji kabla ya utekelezaji kwa dhati.