Mwili wa mwanamme asiyejulikana Ulipatikana na kuopolewa kutoka mto Yala eneo la Bondo kaunti ya Siaya usiku wa Alhamsi.
Mwili huo umepatikana mida ya saa kumi na mbili jioni na familia ambayo ilikuwa inasaka jamaa yao aliyekuwa ametoweka na aliyekuwa ameripotiwa kuzama katika mto huo wiki chache zilizopita.
Chifu wa eno la Got Agulu Joseph Owigo amedhibitisha tukio hilo na kusema kuwa mwili huo wa mtu mwenye miraba mine na urefu wa kadiri, ulikuwa na umekatwakatwa vibaya begani na miguuni.
Kulingana na chifu huyo, tayari mwili huo umesafirishiwa hadi katika hifadhi ya maiti ya hospitali ya Afulu kwa ukaguzi na kutambuliwa huku maafisa wa polisi wakianzisha uchunguzi kuhusu tukio hilo.
Wenyeji wa eneo hilo la Git Agulu na kaunti ya Siaya kwa ujumla, ambao wamewapoteza wapendwa wao kwa njia tatanishi wameombwa kutembelea hifadhi hiyo kuona iwapo mwili huo ni wa jamaa yao.
Tukio hilo linajiri takribana miezi saba baada ya mili 30 zinazokisiwa kuwa za watu waliouawawa kwa mtutu wa bunduki na kitengo cha polisi kilichopigwa maarufuku na serikali ya sasa kupatikana katika mto huo.
Idadi kubwa ya mili hiyo bado haijatambuliwa hadi kufikia sasa kwa mujibu wa taarifa za polisi.