Familia ya mmoja ya waliopigania Uhuru nchini Kenya Dedan kimathi sasa inaitaka serikali ya Rais Wiliam Ruto kuwasaidia ili wapate mabaki ya mpendwa wao ili wakati mke wake Mukami Kimathi atakapofariki atazikwa kando yake.
Wakizungjmza katika kumbukumbu ya 66 ya Dedan kimathi katika uwanda wa Ruringu,mwanawe Dedan Kimathi,Everlyne Waniugu anasema kuwa inahuzunisha zaidi baada ya miaka sitini babake kufariki mabaki yake bado hayajapatikana.
“Kwetu sisi kama Familia tuna hofu sana ikizingatiwa kuwa mama yetu Mukami Kimathi anaugua na siku zake zinazidi kuhesabika kabla ya kufariki kwake,tunazidi kujiuliza iwapo atafariki tutaweza kumzika kando ya bwana wake ambaye kaburi lake hadi leo halipo?” alisema Wanjugu.
Wanjugu anasema kuwa wanaimani kuwa serikali ya Rais William Ruto itaweza kuwasaidia katika jitihada za kupata mabaki ya baba yao ili wayazike kwa heshima inayostahili.
Kimathi alikamatwa wakati wa wakoloni nchini kenya mwaka 1956 katika kijiji cha Karunaini kaunti ya Nyeri na kunyongwa katika gereza la Kamiti ambako alizikwa huku kaburi lake likikosa kujulikana mahali liliko.
Juhudi kutafta alizozikwa Dedan Kimathi hapo awali zimeishia kugonga mwamba