Idadi ya visa vya UVIKO 19 vilivyothibitishwa Afrika vimefikia milioni 1.8 kufikia Jumamosi 18 Septemba, Kituo cha Afrika cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (Africa CDC) kimesema. Idadi ya vifo kutokana na UVIKO 19 imefikia 206,202, na watu 7,454,718 kote barani wakiwa wamepona.
Afrika Kusini, Morocco, Tunisia na Ethiopia yakiwa mataifa yanayoongoza kwa idadi ya visa vya maambukizi ya UVIKO-19 Afrika. Maeneo ya Afrika Kusini yameathriki pakubwa na ugonjwa huo, ikifuatiwa na maeneo ya kaskazini kwa Afrika na Afrika Mashariki, ilhali Afrika ya kati ikiwa haijaathirika pakubwa na UVIKO 19 kulingana na Afrika CDC.