Mtu mwenye nguvu zaidi duniani Iron Biby kutoka Burkina Faso amevunja rekodi ya kuinua chuma cha uzito wa 229 kg. Cheick ’Iron Biby’ Sanou alizaliwa nchini Burkina Faso 1992, akiwa na umri mdogo Biby alipenda michezo kama vile mpira wa vikapu,riadha na mazoezi.Alianza kunyanyua mizani akiwa na umri wa 21, alipoingia shindano lake la kwanza na kushinda.
Mashindano ya “World Log Lift championships” hufanyika kila mwaka na hushirikisha wanariadha wenye nguvu zaidi kutoka mataifa tofauti duniani. Mashindano hayo hujumuisha uinuaji wa magogo ya chuma yenye uzito wa juu.
Iron Biby ameshiriki shindano la “World Log lift Iron” mwaka wa 2018, 2019 na 2021, na anashikilia rekodi ya mwaka 2018 na 2019. Baada ya kuvunja rekodi ya mwaka huu, Iron Biby anashikila rekodi ya Guiness kwa kunyanyua uzito wa juu wa 229 kgs.
Mashindano ya mwaka huu ya “World Log Lift Championships” yalifanyika nchini Scotland 18 Septemba.
Iron Biby, alikaribishwa kwa mbwembwe na shangwe na mashabiki wake alipowasili katika uwanja wa ndege wa Ouagadougou, Burkina Faso