Mtaala wa Elimu ya 8-4-4 Yafikia Kikomo Kenya

Mitihani ya kitaifa ya darasa la nane KCPE na tathmini ya gredi ya sita ya KPSEA ya mwaka huu, imekamilika rasmi.

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE wa mwaka huu ndio wa mwisho katika mtaala wa 8-4-4, ambao umedumu miaka 38. Ilianzishwa mwaka wa 1984

Leo Jumatano, wanafunzi wa darasa la nane walikamilisha mtihani wao wa mwisho kwa kufanya somo la jamii (Social studies).

Kumalizika kwa 8-4-4 kunapisha Mtaala wa CBC (Competency-Based Curriculum) yenye mfumo wa 2-6-6-3. Hii ina maana kuwa mwanafusi atatumikia miaka miwili shule ya chekechea, miaka 6 shule ya msingi, miaka 6 shule ya upili na miaka mitatu chuo kiku.