Cardi B Awasilisha Barua Ya Talaka

Rapa wa kike wa Marekani, Cardi B, kwa mara nyingine tena amewasilisha Barua ya talaka dhidi ya mme wake ambaye ni msanii wa rapa, Offset  takriban miaka saba wakiwa kwenye ndoa.

Mwakilishi wa Cardi B alithibitisha siku ya Alhamisi, 1 Agosti 2024, kuwasilishwa kwa stakabadhi hitajika siku ya Jumatano.

Chanzo cha hatua ya Cardi B yameripotiwa kuhusishwa na masuala ya Kucheza Kamari ya Offset miongoni mwa maswala mengione ambazo hazijawekwa bayana.

Wasanii hawa wa kimarekani wametawala vyombo vya habari tangu 2017, walipotangaza Julai kwamba walikuwa wanatarajia mtoto kabla ya kufunga ndoa mnamo Septemba 2017. Julai 2018, walimkaribisha binti yao, Kulture.

Cardi B, 31, na Offset, 32, wana watoto wawili: binti Kulture, 6, na mdogo wa Kiume,  Wave, 2. Offset pia ni baba wa Jordan, 14, pamoja na Kalea na Kody, wote 9, kutoka kwa mahusiano ya awali.

Hili sio jaribio la kwanza la Cardi B kuwasilisha barua ya talaka. Mnamo Septemba 2020, wanandoa hao walipeana talaka baada ya kutofautiana 2018.

Baadyae waliamua kurudiana pamoja mnamo 2021 na kwa mara nyingine tena Cadi B akatangaza kwamba alikuwa anatarajia mtoto wao wa pili, ambaye walimkaribisha mnamo Septemba 2022.

Kwa sasa Cardi B anatafuta malezi ya msingi ya watoto wao kwa familia ya awali ya offset