Watu wanne wanaotuhumiwa ‘kutumwa na afande’ kumlawiti na kumbaka binti mkazi wa Yombo Dovya, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu Agosti 19, 2024 wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashtaka mawili.
Watuhumiwa wanakabiliwa na kesi ya kubaka na kulawiti na baadae picha mjongeo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuzua hakaruki.
Watuhumiwa hao waliofikishwa mahakamani ni Clinton Honest Damas maarufu Nyundo, Amin Lord Lema ,Nickson Idala Jackson na Playgod Edwin Mushi Kwa mujibu wa taarifa ya Renatus Mkude, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Taifa ya Mashtaka amesema kesi hiyo itasikilizwa kwa siku tano kuanzia leo Agosti 19 hadi Agosti 23 siku ya Ijumaa.
Hata hivyo wanne hao wamekana mashtaka yote mawili yanayowakabili na kurejeshwa Mahabusu hadi kesho shauri hilo litakapoendelea.
“Kutokana na usalama wa Watuhumiwa hawajapata dhamana hivyo wataendelea kuwa ndani huku shtaka likiendelea kusikilizwa na kesi itasikilizwa na siku 5 , Wanajamii wawe Watulivu wakati sheria inachukua mkondo wake, tunaamini haki itatendeka” Renatus Mkude