Kundi moja la vijana na wanaharakati mapema leo asubuhi waliandaa maandamano ya amani mjini Kampala nchi Uganda kupinga mpango wa kujenga bomba la mafuta la Afrika Mashariki (EACOP) kutoka eneo la ziwa Albert hadi bandari ya Tanga Tanzania.
Kundi hilo lilikuwa likiandamana kuelekea katika ofisi ya Waziri Kawi Bi Ruth Nankabirwa kuwasilisha malalamishi yao
Hata hivyo maandamano hayo yalitibuka baada ya polisi wa kupambana na ghasia kuwasili na kuwatawanya maramoja
Baadhi yao wamekamatwa na kwa sasa wanazuiliwa katika seli ya polisi ya central mjini kampala
Madhumuni ya kufanya maandamano kutaka mpango wa kutengezeza bomba la mafuta usimamishwe kwa madai inaharibu mazingiza na pia kuna watu ambao wameathtirika na mpango huo kwa kutolipwa fidia.
Bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Kabaale, linakusudiwa kusafirisha mafuta yanayozalishwa kutoka eneo la Ziwa Albert nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania ambapo mafuta hayo yatauzwa katika masoko ya kimataifa.
Ujenzi wake haujaanza lakini baadhi ya watu wanaoupinga wanasema utaathiri vibaya mazingira.