Je, Raila Ataweza Kunyakua Kiti Cha AUC?

Raila Odinga

Rais wa Kenya, Dkt. William Ruto amemuidhinisha rasmi mpinzani wake wa muda mrefu Raila Odinga katika nafasi ya mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).

Katika hafla iliyoandaliwa katika Ikulu ya Rais jijini Nairobi, iliyohudhuriwa na viongozi kadhaa wa kimataifa akiwemo, rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu, Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni, aliyekuwa rais wa Nigeria, olusegun Obasanjo, pamoja na wawakilishi wa mataifa ya Afrika Mashariki, ikiwamo taifa la Rwanda Rwanda, Rais William Ruto alimsifia Raila kuwa kiongozi wa pekee ambaye anaifahamu Afrika.

“Raila Odinga ana uwezo wa kitaaluma na uzoefu na rekodi iliyothibitishwa ya uongozi wa mabadiliko. huwa anadhamini sifa za kuwa  Pan-African mwenye bidii” – Rais William Ruto alisema.
Kauli ya Rais Ruto aliungwa mkono na viongozi mashuhuri nchini Kenya wakiwemo Naibu wake, Rigathi Gachagua, pamoja na Katinu Mkuu wa Baraza la Mawaziri, ambao walisema kuwa Raila ndiye kiongozi wa pekee nchini Kenya ambaye wamemfadhalisha kuwakilisha taifa la Kenya kimataifa.

Kenya linaendesha kampeni kwa udi na uvumba ya kuhakikisha Raila anajivunia kiti hicho cha uenyekiti wa AUC.

Fuatilia taarifa hiyo kwa kina: