Wanaharakati Uganda waandamana wakiwa uchi

Kundi moja la wanaharakati nchini Uganda leo wamefanya maandamano ya kupinga ufisadi katika taifa hilo. Hata hivo kundi hilo la wanawakwe walifanya maandamano ya kushangaza baada ya kutokezea barabarani wakiwa nusu uchi kama wamebeba mabango yenye maandishi tofauti

Waandamanaji, ambao walikuwa wakiandamana dhidi ya ufisadi bungeni wakiwa wamevua nguo zote na kusalia na suruali za ndani (Underwear).

Walikuwa wamebeba mabango yenye maandshi mbali mbali ya kukemea ufisadi na Rushwa Pamoja na ubadhirifu wa mali ya umma. Baadhi ya jumbe hizo zilidai uwajibikaji kutoka kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Jiji la Kampala (KCCA) kuhusu mkasa wa hivi karibuni katika eneo la Kiteezi.

Waandamano hao ambao walikuwa takribani wanawake wasiopungua 7 walivutia hisia kutoka kwa wapita njia na maafisa wa usalama waliokuwa katika barabara ya kuelekea bungeni.

Hata hivyo maandamano yao yalikatizwa pale maafisa wa polisi walipoingilia katiki, kuwazuia na kuwakamata kwa madai ya kusababisha usumbufu mkubwa katika eneo hilo.

Maafisa wa usalama waliingilia kati haraka kudhibiti hali hiyo, kuwakamata waandamanaji na kuwasafirisha hadi eneo lisilojulikana.

Wakili wa haki za binadamu Eron Kiiza waandamanaji wa uchi “wanaonyesha jinsi rushwa ilivyo uchi” na mafisadi nchini Uganda.

“Je, serikali inayoongozwa na Kaguta Museveni hatimaye itaona na kushughulikia ufisadi?” aliuliza katika chapisho la X, zamani Twitter.

Bw Kiiza alisema polisi “wanapaswa kuwatafuta mafisadi badala ya kuwatazama wasichana hao walio uchi”.

Mamlaka bado hazijatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo, na utambulisho wa waandamanaji haujawekwa wazi.

Maandamano hayo yalikatiza kwa muda mfupi msongamano wa magari na kusababisha vurugu katika eneo hilo, lakini hali ya kawaida ilirejeshwa muda mfupi baada ya kukamatwa.

 

Tukio hilo limezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii, huku maoni yakigawanyika kuhusu ufanisi na usahihi wa aina hiyo ya maandamano.

Waandamanaji hao wanatarajiwa kukabiliwa na mashtaka, ingawa bado haijafahamika ni hatua gani za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.