Mwanaharakati Morara Kebaso aachiliwa kwa dhamana nchini Kenya

Mwanaharakati wa kisiasa Morara Kebaso ameachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa saa kadhaa kufuatia kukamatwa kwake.


Maafisa hao wa DCI walimkamata kutoka afisi yake iliyoko Kahawa Sukari mnamo Jumatatu, Septemba 30.
Morara ameshtakiwa kwa kosa la udhalilishaji kwa kutumia mtandao kinyume na kifungu cha 27 cha matumizi mabaya ya uhalifu wa mtandaoni.
Alishtakiwa kwa kuchapisha habari za uwongo kuhusu mfanyabiashara David Langat
Hata hivyo, wakili huyo mwenye umri wa miaka 28, aliyegeuka kuwa mwanaharakati hakujibu mashtaka kwani mawakili wake walidai kuwa shtaka hilo lilikuwa na dosari.
Baadaye mahakama ilimuachilia kwa dhamana ya KSh 50,000 pesa taslimu, huku uamuzi ukitarajiwa Oktoba 4.
Kukamatwa kwa morara kulizua mdahalo mkali hususan katika mitandao ya kijamii wakitaka aachiliwe. Pia kukamatwa kwakae kusababisha kundi la vijana kuandaa maandamano nje ya mahakama kuu kushinikiza kuachiliwa kwake
Viongozi kadhaa mashuhuri akiwemo Martha Karua, Eugene Wamalwa, Willis Otieno na Jeremiah Kioni pia walihudhuria kortini kushuhudia kufikishwa kwake mahakamani