Bunge ya Kenya limepokea ombi la kutaka kumuondoa kwa lazima Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua ikidaiwa kuwa amekiuka sheria na katiba
Ombi hilo limewasilishwa katika bunge la kenya na mbunge Mutuse Mwengi, mbunge ikitaka bwana Gachagua aondolewe mara moja
Gachagua anashutumia kwa kukiuka katiba na sheria nyengine za nchini na za kimataifa.
Aidha katika ombi lililowasilishwa bungeni, naibu rais anashtumiwa kwa kutomheshimu Rais.
Muswada huo unamtuhumu Naibu Rais kwa kukiuka sheria ya uendeshaji wa serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi. Anadaiwa kuwa katika mkutano wa hadhara akiwachochea wananchi dhidi ya maagizo halali ya jiji la nairobi. Pia anatuhumiwa kutoheshimu viongozi wa mahakama nchini kenya.
Muswada huo vile vile unadai kuwa Naibu Rais amejipatia mali nyingi zaidi kuliko mapato yake kwa kipindi cha miaka miwili ambayo amekuwa ofisini.
Inadai kuwa kwa miaka miwili iliyopita, Gachagua amejipatia mali yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 5.2 ilhali mapato yake ya kila mwaka ni takriban shilingi milioni 12 .Muswada unamshutumu kwa kupata mali hii kupitia njama zake na mke wake na watoto wake.
Pia Muswada huo unamshutumu Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kutoa matamashi yasiyo ya heshima kwa Mkuu wa Mamlaka ya Ujasusi kenya Noordin Hajji
Licha ya tuhuma hizo, Naibu Rais amesema kuwa amejiandaa kwa uamuzi wowote utakaotolewa dhidi yake.
Haya na mengineyo yanamkumba huku Rais William Ruto akiwa kimya.