Maandamano mapya ya kupinga gharama ya maisha yafanyika Nigeria

Nigeria inatarajia kushuhudia maandamano mapya hii leo Jumanne wakati wananhi watapokusanyika kupinga gharama ya maisha.Maandamano hayo yaliyopewa jina la ‘Bila woga Oktoba 1’ yamepangwa kuendana na maadhimisho ya miaka 64 ya uhuru wa Nigeria ambayo yanaadhimishwa Jumanne, Oktoba

Protesters carrying a large Nigerian flag run for safety after Nigerian policemen fire teargas at demonstrators during the “Fearless In October” protest over bad governance in Abuja, Nigeria on October 1, 2024. (Photo by Kola Sulaimon / AFP)

Waandalizi waliviambia vyombo vya habari kuwa maandamano yatafanyika katika mji mkuu Abuja, mji wa bandari wa Lagos na katika miji mikuu ya majimbo katika nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.

 

Maandamano kama hayo yalitikisa Nigeria miezi ya Julai na Agosti, huku waandamanaji wakidai kurejeshwa kwa ruzuku ya mafuta, na kukomesha ufisadi serikalini.

 

Polisi waliwakabili waandamanaji katika maandamano ya awali mjijini Abuja, Nigeria.

Polisi waliwakabili waandamanaji katika maandamano ya awali mjijini Abuja, Nigeria. REUTERS – Marvellous Durowaiye

Takriban watu 22 waliuawa katika msako mkali wa vikosi vya usalama, kulingana na wanaharakati.

 

Katika siku yake ya kwanza ofisini, Rais Bola Tinubu alimaliza ruzuku ya mafuta iliyodumu kwa miongo kadhaa ambayo ilisaidia kupunguza bei. Serikali yake pia ilipunguza thamani ya sarafu mara mbili, na kusababisha bei ya karibu kila kitu kupanda.

Katika hotuba kwa taifa, Tinubu alitetea sera zake lakini hakutoa majibu kwa waandamanaji