Mfahamu Rigathi Gachagua, naibu wa rais wa Kenya aliyeondolewa madarakani

Geoffrey Rigathi Gachagua Alizaliwa mnamo 1965 katika kijiji cha Hiriga kaunti ya Nyeri, ni mtoto wa Gachagua Reriani na Martha Kirigo. Alijiunga na Shule ya Msingi ya Kabiruini kutoka 1971 hadi 1977 kabla ya kuendelea na Shule ya Upili ya Kianyaga kwa ngazi zake za O na A level . Mnamo 1985, alijiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi, ambapo alihitimu na Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Siasa na Fasihi mnamo 1988.

Deputy President of Kenya, Rigathi Gachagua, gestures as he addresses the media during a press conference at his official residence in Nairobi, on October 7, 2024, ahead of the National Assembly vote on his impeachment motion. – The 59-year-old deputy to President William Ruto is accused of corruption, undermining the government and practising ethnically divisive politics, among a host of other charges. (Photo by LUIS TATO / AFP)

 

Baada ya kuhitimu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi akiwa na Shahada ya Uzamili katika Utawala, Gachagua aliajiriwa kwa muda mfupi katika Wizara ya Mambo ya Ndani na Urithi wa Kitaifa kabla ya kujiunga na Taasisi ya Polisi ya Utawala mnamo 1990. Baada ya kuhitimu kutoka taasisi hiyo, Gachagua aliwekwa katika ofisi ya aliyekuwa  Rais Daniel arap Moi kama Afisa wa Wilaya Cadet kati ya 1991 na 1992.

 

Gachagua kisha akahudumu kama Afisa wa Wilaya katika wilaya za Kakamega, Navakholo, Ng’arua na Laikipia. Kati ya 1999 na 2000, alijiunga na Shule ya Serikali ya Kenya ambapo alihitimu na Diploma ya Juu katika Utawala wa Umma.  Kati ya 2001 na 2006, Gachagua alifanya kazi kama Msaidizi Binafsi wa Uhuru Kenyatta.

Gachagua alichaguliwa kuwa mbunge wa eneo bunge la Mathira, ambalo awali lilishikiliwa na kaka yake Nderithu, katika uchaguzi wa 2017.

Mnamo Mei 15, 2022, aliteuliwa kuwa mgombea mwenza wa mgombea urais wa United Democratic Alliance na William Ruto chini ya muungano wa kisiasa wa Kenya Kwanza.  Na baada ya Muungano wao kushinda uchaguzi wa mwaka 2022, Gachagua aliapishwa tarehe 13 september 2022 na kuwa naibu rais wa pili wa kenya chini ya katiba mpya ya 2010 na makamu wa rais wa 12 tangu kenya kujipatia uhuru wake.

Kwa miaka miwili ambayo amekuwa naibu war ais, Gachagua amekuwa akishutumiwakwa misimamo yake mikali ya kisiasa jambo ambalo liliwa kasirisha viongozi wengi na kusababisha kuanzishwa kwa mchakato wa kumuondoa madarakani.  Tarehe 1 Oktoba 2024, hoja ya kumng’oa madarakani Gachagua ililetwa bungeni na kisha baadae wabunge wakapiga kura kuunga mkono hoja hiyo.

Hoja hiyo baadaye ilipelewa katika bunge la seneti na siku ya tarehe 17 oktoba maseneta walipiga kura na maseneta 53 kati ya 67, walipiga kura ya kumuondoa madaraka. Tayari nafasi yake imechukuliwa na Waziri wa usalama wa ndani Prof Kithure Kindiki.

Hata hivyo Gachagua amekumbwa na kesi kesi kadha ya ufisadi ambapo mahakama moja ya Nairobi ilimuamuru kulipa shilingi milioni 200 kwa kumpata na makosa ya ufisadi.

Rigathi amemuoa  Dorcas Wanjiku Rigathi na wana watoto wawili, Kevin na Keith.