Mahakama Kuu Kenya Yasitisha Makubaliano ya Bilioni Ksh.95 Kati ya KETRACO na Kampuni la Adani Energy Solutions

Mahakama Kuu nchini Kenya imesitisha mkataba wa takriban bilioni Ksh.95 kati ya Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Kenya (KETRACO) na Kampuni la Adani Energy Solutions Limited.

Mahakama Kuu Kenya Yasitisha Makubaliano ya Bilioni Ksh.95 Kati ya KETRACO na Kampuni la Adani Energy Solutions

Jaji Bahati Mwamuye alitoa maagizo ya kihafidhina, kusitisha utekelezaji wa makubaliano hayo huku akitaja kuwa mkataba huo umeibua wasiwasi juu ya usiri, ushiriki wa umma, na kufuata katiba

Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Kenya (KETRACO) ilitia saini mkataba wa Ksh 95.68 bilioni na Adani Energy Solutions Limited mnamo Oktoba 11, 2024.

“Ninafuraha kutangaza kutiwa sahihi kwa Makubaliano ya Mradi kati ya Kampuni ya Usambazaji Umeme ya Kenya (KETRACO) na Adani Energy Solutions Limited leo (Kampuni ya Mradi),” Alisema Waziri wa Kawi na Petroli nchini Kenya, Opiyo Wandayi wakati wa kutia saini Mkataba na Adani Energy.

Kulingana na Wandayi, “Ushirikiano wa Umma na Kibinafsi (PPPs), unaashiria mwanzo wa mpango wa mageuzi wa kuendeleza, kufadhili, kujenga, kuendesha, na kudumisha njia kuu za usambazaji na vituo vidogo kote nchini Kenya.”

Mradi baina ya kampuni ya KETRACO na Adani, unajumuisha njia na vituo vidogo vya upokezaji vya voltage ya juu, kama vile Gilgil-Thika-Malaa-Konza 400kV Double-Circuit Line na Rongai-Keringet-Chemosit 220kV Laini.

Kampuni ya Adani Energy Solutions inatarajiwa kusimamia miundombinu hiyo kwa miaka 30 kabla ya kuirejesha mamlaka kwa KETRACO, ikiwa na lengo la kufanya miundombinu ya umeme nchini Kenya kuwa ya kisasa na kusaidia ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

“Tunaamini mpango huu sio tu utaimarisha miundombinu yetu ya nishati lakini pia kuchangia mabadiliko ya kiuchumi na kijamii ya nchi.” Aliongeza.

Mkataba kati ya KETRACO na Adani uliungwa mkono na Rais wa Kenya, William Ruto, ambaye alisema kuwa makubaliano kati ya Adani Group na Kampuni ya Usambazaji Umeme (KETRACO) yatapunguza mzigo wa ushuru kwa Wakenya na kupunguza utegemezi wa mikopo. Ruto aliangazia kuwa Kundi la Adani linawekeza fedha zake zenyewe, kumaanisha kuwa serikali haihitaji kukopa pesa, hivyo basi kuepuka deni la ziada.

Hata hivyo Mahakama Kuu chini Kenya imesitisha utekelezaji wa mkataba huo kutokana na wasiwasi wa usiri, ushirikishwaji wa wananchi, na kufuata katiba.