Gachagua ataka maagizo ya kuzuia kubanduliwa kwake kutoondolewa

Naibu Rais Rigathi Gachagua aliyebanduliwa na Bunge la Seneti anataka jopo la majaji watatu wa mahakama kuu kutoondoa maagizo yanayozuia kutimuliwa kwake madarakani.

Impeached DP Rigathi Gachagua diagnosed with a heart condition

Maagizo hayo yalitolewa na mahakama moja ya Nairobi na nyingine ya Kerugoya.

 

Kupitia mawakili wake wakiongozwa na Paul Muite, Gachagua anasema kuondoa maagizo hayo kutakuwa ukiukaji mkubwa wa haki zake katika kesi hiyo ambayo anasema ni ya maslahi ya umma.

 

Mawakili hao wameshangaa ni nini kitafanyika ikiwa maagizo hayo yataondolewa na kisha mahakama ibaini kuwa mchakato wa kumuondoa Gachagua madarakani haukufuata sheria.

 

Gachagua sasa anataka maagizo hayo kutoondolewa hadi kesi ya kupinga kutimuliwa kwake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

 

Upande wa washtakiwa umewasilisha maombi mbele ya jopo la majaji hao watatu wakitaka maagizo ya kupinga kutimuliwa kwa Gachagua kufutiliwa mbali.

 

Kesi ya Gachagua inasikilizwa na majaji Eric Ogola, Anthony Mrima na Dkt. Freda Mugambi.

Iwapo maamuzi hayo yataondolewa, Profesa Kithure Kindiki huenda akaapishwa wakati wowote kama naibu rais mpya wa Kenya.