Prof Kithure Kindiki aapishwa rasmi kuwa Naibu Rais

Professa Abraham Kithure Kindiki ameapishwa rasmi kuwa Naibu Rais wa tatu wa Kenya chini ya katiba mpya iliyorasimishwa mwaka 2010.

Kindiki akiandamana na mkewe Joyce amekamilisha kula viapo viwili  akiongozwa na msajili wa idara ya mahakama  Winfrida Mokaya.

Kenya’s new Deputy President, Kithure Kindiki (C) takes oath of office as he’s assisted by his wife Joyce Gatiiria Kithure (R) at the Kenya International Convention Centre (KICC) in Nairobi on November 1, 2024. – Kindiki is an academic turned politician who was thrust into the limelight when he defended his boss President William Ruto at the International Criminal Court.
The 52-year-old millionaire served as interior minister for more than two years before taking over as deputy president on November 1, 2024 following the historic impeachment of his predecessor, Rigathi Gachagua. (Photo by SIMON MAINA / AFP)

Kiapo cha kwanza kilikuwa cha uaminifu huku cha ili kikiwa cha utendakazi katika afisi ya Naibu Rais.

Mbele ya maelfu ya wananchi wa Kenya na rais William Ruto, Kindiki ambaye ni Profesa wa sheria, ameapa kuwatumikia wananchi wa Kenya kwa uaminifu kwa moyo.

“Naapa kuwa mwaminifu kwa watu wa Jamhuri ya Kenya,” Kindiki aliapa siku ya Ijumaa kwenye viwanja vya Jumba la Mikutano ya Kimataifa, KICC, jijini Nairobi.

Kindiki amekula kiapo saa nne na dakika 53 asubuhi katika ukumbi wa KICC.

Katika hotuba yake ya kwanza prof Kindiki amemwahidi rais Ruto kuwa hatomwangusha katika majukumu ya kumsaidia kuliongoza taifa hilo.

“Nitakuwa mwaminifu kwako rais na kuwatumikia Wakenya. Asante sana kwa kunipa heshima ya kutumika,” alisema Kindiki.

 

 

Rais William Ruto, amesema alimteua Kindiki kwenye nafasi hiyo kwa sababu, anamwamini na atatumika kwa ajili ya wananchi wa Kenya bila ubaguzi.

 

“Watumikie Wakenya wote bila ubaguzi.,” Ruto amemwambia naibu wake na kuongeza kuwa atumie maarifa yake kuwasaidia wananchi.

 

Aidha Ruto, amemtaka Kindiki kumsaidia kuwaelewesha wananchi kuhusu miradi ya serikali na maendeleo yanayofanywa na uongozi wake.

 

“Nimekuwa nikizungumzia mipango ya serikali peke yangu kwa miaka miwili iliyopita. Nisaidie katika hilo,” Ruto ameongeza.

 

Kindiki anashika nafasi hiyo wakati huu, wananchi wa Kenya wakikabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo, kupanda kwa gharama ya maisha, nyongeza ya kodi,  mabadiliko ya mfumo wa bima ya afya ya umma kutoka NHIF hadi SHA na matukio ya watu kutekwa.

 

Kabla ya kuwa naibu rais, Kindiki alikuwa Waziri wa mambo ya ndani, lakini pia aliwahi kuwa Seneta wa Tharaka Nithi na Naibu Spika wa Seneti.