Takriban Watu Sita Kamefariki Katika Ajali ya Boti Nchini Angola

Takriban watu sita wakiwemo watoto wawili walifariki katika ajali ya boti kwenye pwani ya mji mkuu wa Angola Luanda, polisi na wahudumu wa dharura walisema, huku juhudi za uokoaji zikiendelea Jumatatu.

Takriban Watu Sita Kamefariki Katika Ajali ya Boti Nchini Angola

Kulingana na ripoti za polisi, meli hiyo iliyokuwa imebeba zaidi ya watu 30 ilikuwa sehemu ya msafara wa baharini wa Kikatoliki katika taifa hilo la kusini mwa Afrika wakati ilipozama kwenye Kisiwa cha Luanda siku ya Jumamosi.

Msemaji Hermenio Cazucuto ameliambia shirika la habari la AFP kuwa watu sita wamefariki na wengine 17 wameokolewa.

“Watu wanne walikuwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya na wengine watatu bado hawajulikani walipo”, aliongeza, akisema kuwa juhudi za kuwatafuta zinaendelea Jumatatu.

Kisa hicho kilitokea takriban maili mbili kutoka pwani ya mji wa bandari.

Msemaji wa idara ya huduma ya dharura ya zima moto Maina Panzu aliambia shirika la AFP kuwa wawili kati ya waliofariki ni watoto wenye umri wa miaka minne na sita.

Hadi sasa chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, ila Panzu alisema “uzembe” kutoka kwa nahodha ndio ulishukiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo, na kuongeza kuwa alitoweka.

Chombo cha habari cha Angola24Horas kiliripoti kwamba mashua hiyo ilikuwa imebeba abiria kupita kiasi na kwamba ajali hiyo ilihusisha mashua ya wavuvi katika eneo lenye “mawimbi mengi”.

Katika taarifa yake siku ya Jumapili, Rais wa Angola Joao Lourenco alituma rambirambi zake kwa “familia zilizoathiriwa moja kwa moja na ajali hii mbaya.”