Idadi ya Vifo Kufuatia Kuporomoka Kwa Jengo Kariakoo, Tanzania Imefikia 16

Waokoaji waliendesha shughuli za ukoajo wa watu ambao bado wamekwama katika vifusi vya jengo lililoporomoka katika mji mkuu wa kibiashara wa Kariakoo, eneo Dar es Salaam, Tanzania siku ya Jumatatu, huku idadi ya waliofariki ikiongezeka hadi 16.

Idadi ya Vifo Kufuatia Kuporomoka Kwa Jengo Kariakoo, Tanzania Imefikia 16

“Shughuli za uokoaji zinaendelea kwa sababu baadhi ya watu bado wamekwama kwenye jengo hilo,” alisema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati wa hafla ya kuwaombea majeruhi hao.

“Tunawasiliana na baadhi ya watu walionaswa na kusikia sauti zao,” alisema na kuongeza kuwa hadi sasa watu 86 wameokolewa.

Jengo hilo la ghorofa nne liliporomoka mapema Jumamosi katika soko la Kariakoo lenye shughuli nyingi.

Majaliwa alisema timu ya wataalam 19 wameteuliwa kukagua majengo ya juu katika eneo hilo.

Vile vile amesema athari ya kuanguka kwa ghorofa ni pamoja na kuharibika kwa mali nyingi, majeruhi wengi na mbaya zaidi ni vifo.

Majeruhi walifikishwa kwenye hospitali mbalimbali za jijini na wengi wao wameruhusiwa huku watano wakiwa chini ya uangalizi wa karibu.

Serikali ya Tanzania imeahidi kugharamia matibabu kwa walioathirika, huku Uchunguzi maalum ukitarajiwa kujua chanzo cha ajali na kumsa

Haijabainika ni kwa nini jengo hilo liliporomoka lakini walioshuhudia waliambia vyombo vya habari kuwa ujenzi wa kupanua eneo lake la biashara la chinichini ulianza Ijumaa.

Tukio hilo limeibua tena ukosoaji juu ya ujenzi usio na udhibiti katika mji wa Bahari ya Hindi wenye zaidi ya watu milioni tano.

Moja ya majiji yanayokuwa kwa kasi duniani, Dar es Salaam kumekuwa eneo la kushamiri kwa mali na majengo kuporomoka haraka.

Mnamo mwaka wa 2013, jengo la ghorofa 16 liliporomoka katika jiji hilo na kuua watu 34.