Dkt Philip Mpango aandika barua ya kujiuzulu umakamu wa rais Tanzania

Rais Samia alitangaza kujiuzulu kwa Dkta Philip Mpango kutoka wadhifa wake kama Makamu wa Rais.

Rais Samia alisema, Dkt Mpango alimwandikia barua kutaka kujiuzulu ili akapumzike.

 

”Anasema yeye sasa ana miaka 68 na angependa kuishi zaidi kwa hiyo naomba nipumzisheni, nikambishia bishia wiki iliyopita, lakini hapa akanikabidhi barua yangu hii, sikumjibu, lakini nilipoenda kwa kamati kuu nikawaeleza hiyo hali na kwa pamoja wote tukakubali tumpumzishe,” aliongeza Dkt Samia.

 

Hakuna sababu rasmi zilizotolewa za Dkt Mpango kutaka kujiondoa kutoka wadhifa huo, ila Rais Samia alitaja kuwa hazikuwa sababu za kazi.

Dkt Mpango aliwahi kudokezwa kuwa angewania nafasi ya Makamu wa kwanza mwenyekiti wa Tanzania Bara, japo mwenyewe alipuuza madai hayo katika hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa CCM uliofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dodoma.

Hata hivyo Dkt Mpango ataenelea kuhudumu kama makau war ais hadi pale muda wake utakapokamilika mwezi November mwaka huu.

Rais Samia alitangaza hayo wakati wa mkutano wa kamati kuu ya CCM kilifanyika siku ya jumamosi na jumapili ya tarehe 18 na 19 mwezi huu jijini Dodoma.