Jaji aagiza Dkt Kizza Besigye arejeshwe Gerezani

Mwanasiasa maarufu wa upinzani nchini  Uganda Daktari Kizza Besigye amefikishwa katika mahakama kuu mjini Kampala kusikiliza ombi la mawakili wake la kumtaka achiliwe huru.

Uganda’s veteran opposition figure Kizza Besigye stands in the dock at the Makindye Martial Court in Kampala, on November 20, 2024. – Leading Ugandan opposition figure Kizza Besigye appeared in a military court in Kampala on November 20, 2024 after his reported abduction in neighbouring Kenya. (Photo by Badru Katumba / AFP)

Besigye ambaye amesusia chakula tangu wiki iliopita alionekana kudhoofika huku akiandamana na mshtakiwa mwenzake Haji Obeid Lutale.

Awali jaji wa Mahakama kuu aliaamrisha wandishi Habari kuondoka nje ya kikao cha mahakama na baada ya kufanya mkutano wa faragha na upande unaomtetea Besigye, wandishi habari walirejea kwenye kikao hicho.

Douglas Singiza, Jaji wa Mahakam kuu ya Uganda ameagiza maafisa wa gereza kuwarejesha Besigye na Lutale gerezani, kutokana na kudhoofika kwa afya yake.

Uganda’s veteran opposition figure Kizza Besigye stands in the dock at the Makindye Martial Court in Kampala, on November 20, 2024. – Leading Ugandan opposition figure Kizza Besigye appeared in a military court in Kampala on November 20, 2024 after his reported abduction in neighbouring Kenya. (Photo by Badru Katumba / AFP)

Kwa sasa kikao cha Mahakama kinaendelea bila wawili hao. Mawakili wanaitaka Besigye aachiliwa kwa misingi ya matibabu

Jaji huyo ameagiza Besigye na mshtakiwa mwenzake kurejeshwa gerezani. Jana Waziri wa sheria na masuala ya Kikatiba Nobert Mao aliliambia bunge kuwa Mahakama kuu ya Uganda itaanza mchakato wa kusikiliza ombi la mawakili wa Mwanasiasa huyo ungeanza leo, badala ya Juma nne ya wiki ijayo kama ilivyokuwa imepangawa awali.

Wakili wa Besigye Eron Kiiza ambaye awali alihstakiwa na kuhukumiwa miezi tisa jela na mahakama ya kijeshi, pia amefikishwa mahakamani.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni kupitia mtandao wake wa X jana alishtumu Mahakama kuu zaidi nchini humo kwa

Kuchelewesha mchakato wa kesi ya mwanasiasa huyo wa upinzani ilipotoa uamuzi wa kuivua mamlaka ya kisheria Mahakama ya kijeshi kusikiliza kesi za raia wa kawaida.