Wizara ya Biashara na Ugavi ya Sudan imepiga marufuku mara moja bidhaa zote zinazoingizwa nchini humo kutoka Kenya ikisema kuwa ni kutokana na suala la wasiwasi wa usalama wa kitaifa juu ya Kenya kuunga mkono vikosi vya Rapid Support Forces (RSF), wanachokishtumu kwa kujaribu kuanzisha serikali mbadala.
‘’Uagizaji wa bidhaa zote zinazoingia kutoka Kenya kupitia bandari zote, vivuko na viwanja vya ndege utasimamishwa kuanzia leo hadi siku isiyojulikana,’’ Agizo hilo lilitiwa saini na kaimu Waziri wa Biashara Omar Ahmed Mohamed.
Sudan ilitangaza kuwa itachukua hatua kali dhidi ya serikali ya Kenya kwa kukaribisha vikosi vya RSF jijini Nairobi kufanya mkutano wao.
Hata hivyo, Kenya ilijitetea kuwa haijakiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa, misingi ya Umoja wa Afrika wala Mkataba wa kuzuia uhalifu wa Kimbari kama inavyodaiwa na Sudan.
“Msimamo wa Kenya uko wazi: tunatoa nafasi ya mazungumzo, bila kuchukua upande wowote, kwa sababu tunaamini katika uwezo wa mazungumzo ya amani kutatua mizozo ya kisiasa,” ilisema taarifa ya Kenya.
Kenya ambayo imekosolewa kwa kuruhusu RSF ilisema lengo lake ni kutoa fursa kwa vikosi vya RSF pamoja na mashirika ya kiraia ya Sudan kujadili na kutafuta njia ya kurudisha utawala wa kiraia nchini Sudan.
‘’Tuna imani kwamba watu wa Sudan wataweza kupata suluhu ya haraka na endelevu kwa mgogoro huu,’’ tamko la serikali ya Kenya ilieeleza.
Kenya yaijibu Sudan kuhusu uwepo wa waasi wa RSF jijini Nairobi
Sudan yalaani vikali hatua za Kenya na kuishtumu kwa kukaribisha kundi la RSF