Bingwa wa marathon Eliud Kipchoge ndiye balozi maalum michezo ya Olimpiki Paris 2024

Bingwa wa Marathon Eliud Kipchoge, ameteuliwa kuwa balozi maalum wa michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris Ufaransa.

0
Eliud Kipchoge

Mshindi mara mbili wa nishani ya dhahabu katika mbio za masafa marefu za Olimpiki Eliud Kipchoge, ameteuliwa kuwa balozi maalum wa michezo ya Olimpiki ya 2024 mjini Paris Ufaransa.

Eliud Kipchoge alitangaza hayo jana kwenye ukurasa wake wa Twitter, hii ikimaanisha kuwa atashiriki tena katika mbio hizo za masafa marefu 2024.

Katika majukumu yake kama balozi anatarajiwa kushiriki mbio maalum za kuashiria siku 1000 kabla kuanza kwa michezo hiyo ya Paris 2024. Mbio hizo zitakuwa za 5km na atakuwa anashindana na wanariadha wengine 2000 mjini Paris Oktoba 31.

Mbio hizo zinatumika kuwapa chipukizi nafasi ya kumshinda Eliud Kipchoge ili waonyeshe weledi wao kwenye riadha na kupata nafasi ya kushiriki katika mbio za masafa marefu za Paris 2024.

Kulingana na Kipchoge, atakuwa anakimbia mwendo mrefu zaidi na chipukizi yeyote atakayeweza kwenda sambamba na yeye au hata kumpiku atapata nafasi ya kushiriki mbio za marathon za Paris 2024.

Eliud Kipchoge mwenye umri wa miaka 36 ndiye mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za masafa marefu za Berlin 2018 na Tokyo Japan mwezi Agosti.

Ikumbukwe kuwa nyota huyo wambio alivunja rekodi ya mbio za masafa marefu kwa kukimbia 42.195 KM chini ya saa mbili. Mnamo Oktoba 12 2019 Kipchoge alivunja rekodi ya kukimbia marathon chini ya saa mbili kwa 1:59:40:2 katika shindano la INEOS 1:59.

Eliud Kipchoge

Mbio hizo zilifanyika mjini vIenna na Kipchoge akawa mwanadamu wa kwanza kabisa kukamilisha mbio hizo za 42.195KM chini ya saa 2.

Mbio maalum za kuashiria siku 1000 kabla kuaza kwa michezo ya Olimpiki ya Paris 2024 zitafanyika katika barabara ya Champs-Elysees mjini Paris.

“Kwenye barabara ya kuvutia zaidi duniani, nakupa changamoto njoo ujaribu kunishinda katika mbio hizi, ila bora nisikushinde!” Eliud Kipchoge.

Eliud Kipchoge

In this article

East Africa Premier News Source with Top Stories, Special Features and more.
Uncensored & Undaunted