Boniface Mwangi na Agather wasimulia walivyo bakwa na kudhalilishwa Tanzania

Wakati mkenya Boniface Mwangi  na mwenzake wa Uganda  Agather Atuhaire walipoondoka katika nchi zao Mei 18, 2025, walikuwa na matumaini ya kumuuona na kumpa motisha  mwenyekiti wa Chadema  na kiongozi wa upinzani Tanzania Tundu Lissu, anayeshtakiwa kwa kosa la uhaini.

Kilichokusudiwa kuwa safari ya kawaida ya kuhudhuria kikao cha mahakama na kurudi nyumbani kiligeuka kuwa mateso mikononi mwa maafisa wa polisi wa Tanzania pamoja kundi la wahuni

Boniface na Agather walichukuliwa kwa nguvu kutoka hoteli moja walimokuwa wakiishi Jumatatu, Mei 18, na kupelekwa kwenye vituo vya polisi na kuhojiwa  na maafisa wa uhamiaji na kukabidhiwa kwa mamlaka ya Tanzania .

Katikataarifa  yao kwa vyombo vya habari siku ya Jumatatu, Bony na Agather walisema shambulio hilo lilianza katika kituo cha polisi siku ya Jumatatu, mbele ya mawakili wao.

Akiwa katika ofisi za uhamiaji, Bony anasema alipigiwa simu na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, ambaye alimweleza kuwa atafurushwa Dar es salaam. “Nilisema ninafurahi kurudi nyumbani.”

Hilo halikufanyika, kwani dakika chache baadaye walipelekwa kituo cha polisi ambako walinzi wa serikali walianza kumpiga wakisema alikuwa na lengo la kuiangamiza na kuzua na kuzua vurugu Tanzania.

“Tulihamishiwa kituo cha polisi ambapo tulimkuta kijana anayeitwa Mafwele. Kipigo kiliendelea mbele ya mawakili watatu. Katika kituo hicho, Mafwele alisema anakwenda kumbaka Agather. Wanasheria walipotuacha hawakusema familia zetu kuwa tunapigwa, tunatishiwa na kunyanyaswa, kwa sababu Mafwele mbele ya mawakili aliuliza kama nilitahiriwa, alisema watanitahiri tena.” ,” Boniface alieleza

 

Katika kituo cha polisi cha Central, genge lisilojulikana liliingia ndani. Wanaharakati hao walifunikwa macho na kusukumwa ndani ya gari aina ya Landcruiser ambalo liliondoka kwa takriban dakika 20. Wakaingizwa kwenye chumba ambacho kikawa chumba chao cha mateso.

“Waliniambia nivue nguo, nilipovua walinitoa pingu, nikashikwa na wanaume karibu wanne, wakaninyanyua kwa kasi na kunifunga kichwa chini, wakaanza kunipiga miguu, wakaniwekea chupi mdomoni, wakacheza muziki wa injili ndani ya gari ili kudidimiza maumivu yangu,” alisema Bonifcae.

Anasema wakati huo alinajisiwa, huku wakisema maneno ya kumsifu rais Samia. Unyanyasaji wa kijinsia ulikuwa sawa kwa wanaharakati wote wawili, ambao walikuwa na vitu vilivyoingizwa kwenye sehemu yao ya makalio.

“Waliniuliza niseme ninajisikia vizuri, na kusema ‘Asante Samia’. Nilianza kutokwa na damu. Wakati huu wote wanasema wanarekodi kile wanachonifanyia,”alisema Boniface.

Agather alieleza kwamba watesaji walitumia vitu vingine kuwanyanyasa kingono na wala si viungo vyao vya ngono. Huku wakiwa wamefungwa pingu mikononi na kufumba macho, maumivu yalikuwa kwa vingi kwenye miguu yao

“Watu walikuwa wamekuja na maagizo moja. ‘hakikisheni wanapata maumivu mengi muwezavyo,” Agather alisema. Baada ya mateso hayo, walikaa Jumatatu usiku kwenye ghorofa yenye baridi kabla ya kuhamishwa kando hadi eneo tofauti Jumanne asubuhi.

“Sikujua nilikokuwa lakini nilisikia wito wa maombi. Walikuja kunitukana na kuondoka. Jumatano asubuhi walinipa kikombe cha chai na mandazi,” Bony alisema.

“Mateso ya kisaikolojia ya masaa hayo ya kuendesha gari yalikuwa mabaya zaidi kuliko mateso ya kimwili. Niliendelea kufikiria walikuwa wakitupeleka kwenye bustani ili kuliwa na wanyama, wakati mwingine nilisikia bahari ikiunguruma na nilifikiri watatutupa baharini,” Agather alisimulia.

Katika vyumba vya mateso, dozi za dawa za kutuliza maumivu zilitolewa kwa wanaharakati.

Bony alikumbuka kuwa siku ya Alhamisi asubuhi, alikimbizwa hadi eneo la mpaka ambapo kulikuwa na bodaboda akisubiri kumsafirisha hadi Kenya. Huko, alipewa Tsh.20,000 na Ksh.400 kwa ajili ya usafiri wake.

Agather pia alimtaja Faustine Mafwele kuwa ndiye aliyeamuru genge hilo kuwavamia.