DR Congo yafuzu kushiriki kombe la dunia

Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imefuzu kwenye fainali ya kombe la dunia, kwa mara ya kwanza, baada ya miaka 52, baada ya kuifunga Jamaica bao 1-0, katika mechi muhimu ya kufuzu iliyochezwa kwenye uwanja wa Guadalajara nchini  Mexico, Jumanne tarehe 31, 3 2026

ZAPOPAN, MEXICO – MARCH 31: Axel Tuanzebe of Congo DR celebrates after scoring the team’s first goal during the FIFA World Cup 2026 Play-Off tournament final match between Congo DR v Jamaica at Estadio Guadalajara on March 31, 2026 in Zapopan, Mexico. Agustin Cuevas/Getty Images/AFP (Photo by AGUSTIN CUEVAS / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via AFP)

Bao la ushindi lilifungwa katika muda wa ziada na Axel Tuanzebe, beki wa zamani wa Manchester United, katika mechi hiyo ngumu, iliyoishi kwa DRC kuandikisha historia nyingine ya kurejea tena kwenye michuano hiyo mikubwa na kuleta furaha kubwa kwa mashabiki na raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ushindi wa DRC unamaanisha kuwa, bara la Afrika litakuwa na wawakilishi 10 katika michuano hiyo inayoanza kutifua vumbi mwezi Juni hadi Jumai katika nchi za Marekani, Cananda na Mexico.

DRC ilifika hatua hii baada ya kuifunga Nigeria katika mchuano muhimu kati ya timu za Afrika na baadaye kufuzu katika fainali na kukutana na timu kutoka bara lingine, ili kutafuta nafasi hiyo ya kufuzu.

Timu hiyo sasa inajiunga na Ureno, Colombia na  Uzbekistan katika kundi moja kuwania kombe hilo la dunia.

Kombe la dunia litaanza rasmi tarehe 11 Juni mwaka 2026 na litaandaliwa katika mataifa matatu, Canada, Mexico na  Marekani