Korea Kaskazini inaonekana kuwakandamiza watu wanaosambaza au kutazama kipindi maarufu cha “Squid Game” cha Netflix.
Ripoti ya kituo cha Radio Free Asia (RFA) ilinukuu vyanzo ambavyo havikutajwa kutoka Korea Kaskazini vikisema mtu aliyesafirisha na kuuza tamthilia hiyo amehukumiwa kifo kwa kupigwa risasi na mwanafunzi wa shule ya upili ambaye alinunua kimenyela USB kilichokuwa na kipindi hicho alihukumiwa kifungo cha maisha jela.
Wanafunzi wengine sita wa shule ya upili ambao walitazama kipindi hicho walisemekana kuhukumiwa miaka mitano ya kazi ngumu, RFA iliripoti. Wasimamizi wao pia walisemekana kuadhibiwa, walimu na wasimamizi wa shule walifukuzwa kazi.
Kituo cha RFA ni huduma ya habari isiyo ya faida inayofadhiliwa na serikali ya Amerika ambayo inahudumu barani Asia, inasema lengo lake ni “kutoa habari na taarifa sahihi na kwa wakati kwa nchi za Asia ambazo serikali zake zinazuia upatikanaji wa habari.”
Kipindi cha televisheni cha Korea Kusini “Squid Game” kinasimulia hadithi ya watu 456 wenye madeni wakishindania kushinda dola bilioni 45.6, au dola milioni 38.3, za pesa za zawadi katika michezo ya kikatili ya kujiokoa maisha.
Chanzo cha sheria katika jimbo la Hamgyong Kaskazini mwa Korea Kaskazini kiliiambia huduma ya RFA ya Korea: “Haya yote yalianza wiki iliyopita wakati mwanafunzi wa shule ya upili aliponunua kinyemela cha USB kilichokuwa na tamthilia ya Korea Kusini ya “Squid Game” na kuitazama rafiki yake wa karibu darasani.
Rafiki huyo aliwaambia wanafunzi wengine kadhaa, ambao nao waliweka tamthilia hiyo kwenye vimenyela vyao.” Wanafunzi hao walinaswa na wachunguzi wa serikali, chanzo kiliiambia RFA.
Ni mara ya kwanza kwa serikali ya Korea Kaskazini kuwaadhibu watoto chini ya sheria ambayo inaadhibu usambazaji na kutazama habari na vipindi kutoka nchi za kibepari kama vile Korea Kusini na Marekani, RFA ilisema.
“Serikali inalichukulia tukio hili kwa uzito mkubwa, ikisema kuwa elimu ya wanafunzi ilikuwa ikipuuzwa,” chanzo cha RFA kilisema.
Chanzo kimoja kilisema kwamba mmoja wa wanafunzi hao alikwepa kuadhibiwa kwa sababu alikuwa na wazazi matajiri ambao walitoa rushwa ya $ 3,000.
Licha ya tishio la kuadhibiwa nakala za magendo na haramu za “Squid Game” zimekuwa zikiingizwa Korea Kaskazini.
Netflix imesema kuwa tamthilia hiyo imepata umaarufu na utazamaji wa juu katika mwezi wa kwanza ilipozinduliwa kushinda vipindi vingine.