Mfalme wa jamii ya Khoisan nchini Afrika Kusini, ambayo imefanya maandamano kwa zaidi ya miaka mitatu katika majengo ya Union Building mjini Pretoria amekamatwa kwa kupanda bangi.
Mfalme Khoisan alikamatwa na wengine wawili kwa sababu hiyo hiyo.
Kikundi hicho cha watu wa jamii wa Khoisan kimepiga kambi katika mahema mita chache tu kutoka kwenye sanamu ya rais wa zamani Nelson Mandela kwa lengo la kukutana na rais Cyril Ramaphosa kuhusu masuala ya kutambuliwa, ardhi, lugha na kurejesha utambulisho wao.
Mke wa Mfalme Khoisan, Malkia Cynthia alisema mimea ya bangi ambayo mfalme alikamatwa nayo ilikuwa hapo kwa takriban miaka mitatu.
“Idadi kubwa ya polisi waliokuwa na bunduki walikuwepo wakati wa kukamatwa kwa mumewe.
“Mfalme alijaribu kwa kila njia kuwazuia polisi kuchukua mimea hiyo lakini polisi wanne walimtoa nje ya bustani hadi kwenye sanamu ya Nelson Mandela.
“Tumekuwa tukitumia bangi kwa madhumuni ya dawa kwa muda mrefu sana na wagonjwa huja kwetu kila siku kupata matibabu.
Malkia Cynthia pia alisema kuwa wamekasirishwa sana kwamba hakuna mtu kutoka ofisi ya rais ambaye amejisumbua kuzungumza nao.
“Nina hasira sana. Tumekuwa hapa tangu Novemba 2018 na Rais Ramaphosa hajawahi kuchukua hata dakika moja ya wakati wake kutuhutubia au kutambua uwepo wetu lakini sasa wanaleta polisi ili kututesa.
“Hata walivamia kambi yetu wakijaribu kutafuta vitu visivyo halali ili sisi pia tukamatwe.
“Jambo hili limeitia kiwewe familia yetu akiwemo mtoto wetu anayesoma darasa la 9.
Huduma ya Polisi ya Afrika Kusini haikuweza kupatikana kutoa maoni yao kuhusiana na kisa hicho.
Baadhi ya picha alipokamatwa Mfalme Khoisan: