Visa vya UVIKO-19 na idadi ya vifo kutokana na ugonjwa huo vimepungua barani Afrika kwa mara ya kwanza tangu wimbi la nne la virusi hivyo kufikia kilele chake, UN ilisema Alhamisi.
Ikielezea kuzuka kwa ugonjwa huo katika siku 56 kama “wimbi fupi zaidi barani Afrika,” ofisi ya kanda ya Afrika ya Shirika la Afya Duniani ilisema. Visa vipya vilivyoripotiwa vilipungua kwa asilimia 20 katika wiki iliyopita hadi Jumapili, wakati vifo vilivyoripotiwa vikipungua kwa asilimia nane.
Katika taarifa iliyotolewa baada ya mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari, ofisi hiyo pia ilisema Afrika Kusini, ambapo kirusi cha Omicron kiligunduliwa kwa mara ya kwanza, imeshudia kupungua kwa visa vya UVIKO 19 katika wiki nne zilizopita.
Ni Afrika Kaskazini pekee iliyoripoti ongezeko la visa vya ugonjwa huo wiki jana, “visa vya ugonjwa huo vikiongezeka kwa asilimia 55,” ilisema.
Matshidiso Moeti, mkurugenzi wa WHO katika kanda ya Afrika, alionya kuwa “Bara bado halijabadili msimamo wake kuhusu janga hili. Maadamu virusi vinaendelea kusambaa, mawimbi zaidi ya ugonjwa huo hayawezi kuepukika.”
“sio tu kutoa chanjo zaidi, lakini pia kupata matibabu muhimu ya UVIKO -19 ili kuokoa maisha na kupambana na janga hili.”
Asilimia 10 pekee ya watu wa Afrika wamepatiwa chanjo kamili, kulingana na WHO.Bara hili lenye wakazi bilioni 1.2, halijaathiriwa sana na janga hilo, likiripoti vifo 234,913 kutokana na visa milioni 10.5, kulingana na hesabu za AFP.