Notice: Function _load_textdomain_just_in_time was called incorrectly. Translation loading for the wordpress-seo domain was triggered too early. This is usually an indicator for some code in the plugin or theme running too early. Translations should be loaded at the init action or later. Please see Debugging in WordPress for more information. (This message was added in version 6.7.0.) in /home/mwanzotv/public_html/wp-includes/functions.php on line 6114
Madagascar: Kimbunga Batsirai chawaua watu 10 na kuwafanya karibu 48,000 kuyahama makazi yao - Mwanzo TV

Madagascar: Kimbunga Batsirai chawaua watu 10 na kuwafanya karibu 48,000 kuyahama makazi yao

Wakaazi wa kisiwa cha La Reunion wakitazama meli ya mafuta iliyokwama baada ya kupoigwa na kimbunga Batsirai (Photo by Richard BOUHET / AFP)

Kimbunga Batsirai kilisababisha vifo vya takriban watu 10 na kuwafanya karibu 48,000 kuyahama makazi yao wakati kilipopiga Madagascar usiku kucha, shirika la kitaifa la kudhibiti majanga lilisema Jumapili.

Baadaye kimbunga hicho kilidhoofika lakini sio kabla ya kusababisha uharibifu katika nchi hiyo ya kisiwa cha Bahari ya Hindi ambayo bado inakumbwa na athari za dhoruba mbaya ya kitropiki iliyotukia mapema mwaka huu.

Maeneo ya nchi yalikumbwa na mvua kubwa na upepo mkali kabla kimbunga hicho kutua huko Mananjary.

Kimbunga hicho kiling’oa miti na kuharibu majengo. Mvua hiyo itasababisha mafuriko katika sehemu zote za nchi, ofisi ya hali ya hewa ya Madagascar ilisema Jumapili.

Batsirai kilifika nchi kavu Jumamosi jioni kikiambatana na upepo wa kilomita 165 (maili 102) kwa saa, Faly Aritiana Fabien wakala wa kudhibiti majanga nchini humo aliiambia AFP.

Mfanyakazi mwenzake anayehusika na udhibiti wa hatari, Paolo Emilio Raholinarivo, alisema kuwa watu 10 walikufa, lakini hakutoa maelezo zaidi.

Hata hivyo ofisi ya taifa ya hali ya hewa ilisema Jumapili kwamba Batsirai imedhoofika.

Kasi ya upepo wa kimbunga hicho imepungua karibu nusu hadi maili 80 kph, wakati upepo mkali zaidi ukipungua hadi kilomita 110 kutoka kilomita 235 iliyorekodiwa wakati kilipotua, Meteo Madagascar ilisema.

Takriban asilimia 95 ya jiji limeharibika

Mti uliong’olewa na kimbunga Batsirai katikati ya Antsirabe (Photo by RIJASOLO / AFP)

“Mananjary imeharibiwa kabisa, haijalishi popote unapoenda kila kitu kimeharibiwa”, alisema mkazi mmoja anayeitwa Faby. Mwanaume mwingine, Fana, alikuwa na uhakika “takriban asilimia 95 ya jiji limeharibiwa.”

Huduma ya hali ya hewa ya Meteo-Ufaransa ilikuwa imetabiri hapo awali kuwa Batsirai kingekuwa “tishio kubwa sana” kwa Madagascar baada ya kupita Mauritius na kupeleka mvua kubwa katika kisiwa cha Ufaransa cha La Reunion.

Takriban watu 10,000 kutoka La Reunion walikuwa bado hawana umeme siku ya Jumapili, siku tatu baada ya kimbunga hicho cha kitropiki kupita katika kisiwa hicho, na kuwajeruhi watu 12.

Kimbunga Ana kiliathiri takriban watu 131,000 kote Madagascar mwishoni mwa Januari, na karibu watu 60 waliuawa, wengi wao kutoka  mji mkuu Antananarivo.

Ana pia iliathiri Malawi, Msumbiji na Zimbabwe, na kusababisha vifo vya makumi ya watu.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WHO likinukuu makadirio kutoka kwa mamlaka ya kitaifa, lilisema takriban watu 595,000 wanaweza kuathiriwa moja kwa moja na Batsirai, na wengine 150,000 wanaweza kuyahama makazi yao kwa sababu ya maporomoko ya ardhi na mafuriko.