RAIS MPYA WA ZAMBIA AAPISHWA

Hakainde Hichilema – Rais mpya wa Zambia

Hakainde Hichilema ndiye rais mpya wa Zambia. Hichilema amekuwa mfanyabiashara na mwanasiasa kwa miaka mingi, amewania kiti cha urais mara tano 2006, 2008, 2011,2015 na 2016.Katika uchaguzi wa Agosti 2021, alimshinda mpinzani wake Edgar Lungu wa chama cha Patriotic Front katika uchaguzi wa urais kwa 59% ya kura zote zilizopigwa, ameongoza chama cha United Party for National Development tangu 2006.

Katika uchaguzi wa 2006, Hichilema Hakainde aliwania kiti cha urais kwa mara ya tano kwa tiketi ya chama cha UDA akishindania kiti hicho dhidi ya wapinzani wake, Levy Mwanawasa aliyekuwa rais wakati huo kwa chama cha Movement for MultiParty Democracy na Michael Sata wa Patriotic Front.

Mwaka wa 2015, katika uchaguzi mkuu Hakainde aliibuka wa pili, baada ya kupoteza uchaguzi huo kwa kura 27,757 pekee, na Rais Edgar Lungu akaapishwa kama rais wa sita wa nchi hiyo.

Edgar LunguRais wa zamani wa Zambia

Rais Edgar Lungu alichukua uongozi wa Zambia, na miaka miwili baadaye 2017 Hakainde Hichilema alizuiliwa kwa madai ya uhaini na akashtakiwa kwa kujaribu kupindua serikali, alihudumia kifungo cha miezi 4 jela.Agosti 17 2017 kulikuwa na sherehe kubwa sehemu tofauti Zambia baada ya kuachiliwa kwa Hakainde.Agosti 12 2021 Tume ya uchaguzi nchini Zambia ilimtangaza HichilemaHakainde (59) mshindi wa uchaguzi baada ya kumshinda Rais Edgar Lungu kwa zaidi ya kura milioni moja.

Rais Samia Suluhu Hassan

Baadhi ya viongozi waliohudhuria sherehe hiyo ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa wa Botswana Mokgweetsi Masisi, Rais wa Malawi Lazarus Chakwera, Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.