Kupanda kwa bei ya vyakula, iliyosababishwa na uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, kunazua hofu ya njaa na machafuko katika eneo lenye matatizo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Katika iliyo katikati mwa Afrika, robo tatu ya kaya zinaishi chini ya kiwango cha chini cha umaskini.
Lakini hali ya usalama inajitokeza kuwa tatizo kubwa zaidi kaskazini mashariki mwa DRC, ambako uchumi umelemazwa na hali mbali ya kijiografia na miongo kadhaa ya ghasia.
“Mamlaka zinahitaji kuona nini wanaweza kufanya, vinginevyo tutakufa kwa njaa,” alisema Pascaline Buhume, mchuuzi wa chakula huko Bukavu, jiji lililo upande wa kusini mwa Ziwa Kivu ambalo linatenganisha DRC na Rwanda.
Bei ya unga wa mahindi, mchele, sukari, mafuta na nyanya imepanda, na hivyo kutoa changamoto kubwa kwa wale wanoishi kwa dola kadhaa kwa siku.
Gunia la kilo 50 la sukari ambalo awali liligharimu sawa na dola 43 sasa linauzwa dola 60, alisema Buhume.
Mkopo wa kilo 20 wa mafuta ya kupikia sasa unagharimu dola 45 badala ya dola 30, na gunia la kilo 25 la mchele limepanda kutoka dola 18 hadi 20.
Mama wa watoto watano ambaye alikuwa na wasiwasi alidokeza kuwa mkate ambao awali ulinunuliwa kwa 1,000 za Congo sasa unagharimu 1,200.
Janvier Mizo Kabare, ŕais wa kikundi cha haki za wanunuzi chenye makao yake makuu mjini Kinshasa kiitwacho LICOSKI, alisema Bukavu ni sehemu kubwa ya mfumuko wa bei, inayoteseka siyo tu kutokana na “kuyumba kwa bei ya chakula” lakini pia kupanda kwa bei ya mafuta.
Gharama ya wastani kwa tenki la mafuta linaloleta petroli kutoka mpakani imepanda kutoka dola 726 hadi $900, alisema Urbain Kange, katibu wa chama cha sekta ya mafuta cha Bukavu.
“Tunafanya tuwezavyo, lakini wasambazaji wetu wa Tanzania, Rwanda na Kenya wanatuambia kuna uhaba upande wao,” alifafanua.
Vituo kadhaa vya petroli huko Bukavu tayari havina mafuta, na uhaba huo unalazimisha bei kupanda.
“Kupatikana kwa mafuta kunakuwa tabu sana,” alisema Jeremie Cito, dereva wa teksi ya pikipiki.
Sasa analazimika kutoza franc 1,000 kwa muda mfupi ikilinganishwa na 500 hapo awali, aliongeza.
Hali inazidi kuwa mbaya kutokana na ukweli kwamba jimbo hilo linategemea kabisa uagizaji bidhaa kutoka nje, alisema Paulin Bishakabalya, mchambuzi wa uchumi wa Shirikisho la Biashara la Congo (FEC).
Mchele, ngano, mahindi na mafuta vyote vinaweza kuzalishwa ndani ya nchi, alisema.
Eninga Abwe, ambaye anaongoza ofisi ya biashara ya nje ya Bukavu, alisema wakaguzi walikuwa wakitumwa kuangalia masoko kwa ajili ya upandishaji wa bei.
Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine umepata pigo kwa mauzo ya nafaka kutoka nchi zote mbili, ambazo ni wazalishaji wakuu wa ngano na nafaka nyingine.
Bishakabalya alisema kutokuwa na uhakika unagubika soko la nafaka la dunia ulikuwa unawafanya baadhi ya wauzaji “kujilimbikizia bidhaa hiyo” ipande bei pia.
“Serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka,” alisema, akitaka hatua za kuchochea uzalishaji wa nyumbani.
DRC inajivunia rasilimali kubwa ya madini na mamilioni ya hekta (ekari) za mashamba yanayoweza kuzalisha chakula kingi.
Lakini kugeuza ardhi hiyo kuwa kilimo chenye tija kunahitaji mtaji kurekebisha mfumo duni wa usafiri nchini na utashi wa kisiasa wa kushughulikia vikwazo vya kiutawala na vingine.
Kulingana na Benki ya Dunia zaidi ya asilimia 70 ya watu milioni 90 wa DRC wanaishi chini ya dola 1.90 kwa siku.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya Jumatatu kwamba mzozo wa Ukraine ulimaanisha ulimwengu lazima uchukue hatua kuzuia “kimbunga cha njaa na kuzorota kwa mfumo wa chakula duniani.”
Nchi 18 za Kiafrika na ambazo hazijaendelea zinaagiza angalau asilimia 50 ya ngano kutoka Ukraine au Urusi, alisema — na miongoni mwao ni DRC.