Afrika Kusini imesajili jumla ya vifo 100,000 kutokana na UVIKO 19, kulingana na takwimu rasmi zilizotolewa Jumatano, lakini idadi ya vifo vinaaminika kuwa juu zaidi.
Takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Kitaifa ya Magonjwa ya Kuambukiza zilionyesha jumla ya vifo 100,020 vimetokea tangu kuanza kwa janga hilo miaka miwili iliyopita.
Taasisi hiyo iliripoti vifo 44 siku ya Jumatano, vifo sita vikiripotiwa siku mbili zilizopita, wakati wengine waligunduliwa wakati wa ukaguzi wa serikali unaoendelea.
Vifo vilivyotokana na UVIKO-19 vinakadiriwa kuwa juu zaidi kuliko ilivyoripotiwa rasmi, huku watafiti wakisema inaweza kuwa mara tatu zaidi ya takwimu zilizoripotiwa.
Takwimu zilizokusanywa na Baraza la Utafiti wa Kimatibabu la Afrika Kusini zinaonyesha kuwa kumekuwa na vifo zaidi ya 300,000 tangu janga hilo lilipotokea.
“Tangu Mei 3, 2020, kumekuwa na jumla ya vifo 303,400,” baraza lilisema katika ripoti Jumanne.
Data ya vifo vya zaidi inatokana na makadirio ya vifo ambavyo vinaweza kutarajiwa kutokea bila janga, kulingana na mbinu inayotumiwa na kikundi cha utafiti kinachofadhiliwa na serikali .
“Ingawa data zaidi inahitajika juu ya sababu za msingi za kifo vya kawaida , uchunguzi unaunga mkono sana kwamba sehemu kubwa ya vifo vya ziada vinavyozingatiwa nchini Afrika Kusini vinaweza kuhusishwa na UVIKO-19,” ilisema katika ripoti kwenye tovuti yake.
Kwa mujibu wa baraza hilo, vifo 85,000 zaidi vilitokea katika mwaka wa kwanza wa janga hilo, 203,200 vilitokea mwaka jana, wakati zaidi ya 15,000 vimetokea hadi sasa mwaka huu.
Afrika Kusini ndio nchi iliyoathiriwa zaidi barani Afrika kutokana na UVIKO 19, ikihesabu zaidi ya visa milioni 3.7 vya maambukizi ya ugonjwa wa coronavirus ikiwa ni zaidi ya asilimia 30 .
Licha ya hayo Afrika Kusini inapanga kuharibu takriban chanjo 92,000 za Pfizer ambazo zipo karibu kuharibika siku ya Alhamisi, wizara ya afya ilisema katika taarifa.
Itakuwa mara ya kwanza Afrika Kusini ambapo asilimia 30 ya watu wamechanjwa kikamilifu — kutupa chanjo ya Covid, kwani matumizi “yanapungua,”, serikali ilisema.
Dozi nyingine takriban 900,000 zinatarajiwa kuharibika mwezi Mei huku milioni 5.8 zikiharibika mwezi Juni, huku nyingine milioni 4.8 zikifikia tarehe ya mwisho mwezi Julai.
Rais Cyril Ramaphosa wiki iliyopita aliondoa vikwazo vingi vilivyosalia vya kukabiliana na coronavirus huku maambukizo mapya yakipungua na vifo vichache vikiripotiwa.