Hili ni Kombe la Dunia lenye utata zaidi katika historia, huku Qatar ikiwa imezingirwa na utata tangu ilipotangazwa kuwa mwenyeji mwaka 2010 wakishtumiwa kununua kura — ambazo zilikanushwa vikali — na maswali juu ya kufaa kwa nchi hiyo kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia.
Kuanzia masuala ya haki za binadamu hadi vita vinavyoendelea nchini Ukraine, imekuwa vigumu kuweka kipaumbele kwenye mchezo huo pekee, lakini rais wa FIFA Gianni Infantino amerudia, kama alivyofanya siku ya Alhamisi, kwamba “Itakuwa Kombe la Dunia la ajabu na la kipekee.”
“Hatutakuwa na Kombe lingine la Dunia ambapo viwanja vinane viko ndani ya kilomita 50, mashabiki wanaweza kutazama michezo kadhaa kwa siku na timu hazitasafiri muda mrefu kufika viwanjani,” alisisitiza kabla ya Kombe la Dunia la kwanza kuchezwa Novemba na Desemba.
Hatua ya kuondoa mechi hizo kutoka miezi ya kawaida ya Juni na Julai ililazimishwa na kuwepo kwa joto katika eneo hilo wakati huo wa mwaka, lakini mashindano yanakaribia na msisimko wa kandanda hauepukiki.
Droo ya Ijumaa itafanyika katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Doha, huku washindi wa zamani wa Kombe la Dunia kama vile Cafu na Lothar Matthaeus wakiwa kati ya wasaidizi wa droo. Washindi wa mwisho wa Kombe la Dunia Ufaransa itakuwa katika kundi la Kwanza.
Kundi la timu bora litajumuisha mataifa saba ya juu katika viwango vya FIFA na vile vile Qatar wanaoshiriki kwa mara ya kwanza, wakiwa katika nafasi ya 51 kwa ratiba ya FIFA wakijumuishwa kwenye kundi hilo kwa kuwa wao ni wenyeji wa mashindano ya mwaka huu.
Taifa nambari moja duniani Brazil, Ubelgiji, Argentina ya Lionel Messi, Uingereza, Uhispania na Ureno ya Cristiano Ronaldo ndizo zinazoshika nafasi ya kwanza, huku timu hizo zikinufaika na kukosekana kwa mabingwa wa Ulaya Italia.
Hiyo pia inamaanisha Ujerumani, baada ya kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya makundi mwaka wa 2018, ndio jina kubwa zaidi katika Chungu cha Pili, ambacho pia kina Uholanzi na Croatia.
Mabingwa wa Afrika Senegal, Japan na Poland ya Robert Lewandowski ni miongoni mwa timu katika chungu cha tatu, na Canada watakuwa katika chungu cha nne katika mechi yao ya kwanza tangu 1986.
Nafasi tatu bado kuamuliwa
Ikiwa mashabiki wa mataifa 29 yaliyofuzu kutoka pande zote ulimwenguni wakifuatilia kwa hamu droo hiyo, nafasi tatu bado hazijaamuliwa katika Kombe la Dunia la timu 32, kabla ya timu zinazoshiriki Kombe la Dunia kuongezwa hadi timu 48 ifikiapo mwaka wa 2026.
Nchi hiyo ndogo ya Ghuba yenye watu chini ya milioni tatu iliushangaza ulimwengu wakati lilipopewa haki za uenyeji, na imekuwa likijitayarisha tangu wakati huo.
Viwanja saba kati ya vinane vimejengwa hivi karibuni, huku Doha pia ikifungua mfumo mpya wa treni katika maandalizi ya kukaribisha mashabiki kutoka kote ulimwenguni.
Zaidi ya tikiti 800,000 tayari zimeuzwa, na wakati mechi zinaanza ujenzi unapaswa kukamilika kwenye barabara ya Corniche ya Doha.