Waziri wa fedha wa Kenya Alhamisi alizindua bajeti ya dola bilioni 28 inayolenga kusaidia uchumi kuimarika baada ya janga la UVIKO-19 kuwafanya mamia kwa maelfu ya watu kukosa kazi.
Mwongozo wa kifedha wa mwaka wa fedha wa 2022/2023, uliotangazwa miezi minne tu kabla ya nchi kupiga kura, pia unasukuma mabilioni ya fedha katika kile kinachoitwa miradi ya Rais Uhuru Kenyatta na miundomsingi mikuu — mingi ikifadhiliwa na Uchina.
“Tumeelezea sera katika bajeti hii ambazo zinalenga kurudisha uchumi kwenye njia endelevu zaidi ya ukuaji wa maisha bora, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Hazina Ukur Yatani aliambia bunge.
Alisema uchumi wa nchi hiyo unatarajiwa kukua kwa asilimia sita katika mwaka huu kutoka asilimia 7.6 mwaka jana lakini kuimarika kwa kiwango cha asilimia 0.3 mwaka 2020 — cha kwanza katika miongo mitatu.
Kenya iliathiriwa sana na janga la coronavirus, ambalo lilipunguza mapato kutoka kwa sekta muhimu ya utalii, ingawa kilimo – uti wa mgongo wa uchumi – uilithibitika kuwa thabiti zaidi.
“Watu wetu wanateseka” –
Mnamo 2020 zaidi ya watu 700,000 walipoteza kazi zao na Wakenya bado wanatatizika kukabiliana na kupanda kwa gharama za bidhaa za kimsingi kama vile chakula na mafuta huku maeneo kadhaa ya nchi yakikumbwa na ukame.
“Serikali imetufeli, tuna njaa, tunataka chakula, watu wetu wanateseka na wanakufa,” mwandamanaji mmoja alipiga kelele nje ya bunge, wakati polisi walipomkamata.
Bajeti ya shilingi trilioni 3.3 (dola bilioni 28, euro bilioni 26) inaonyesha njia nzuri ambayo serikali injaribu kuboresha maisha ya watu lakini pia kukuza hazina yake kwa kuongeza kodi.
Yatani alitabiri nakisi ya bajeti ya asilimia 6.2 ya Pato la Taifa (GDP), kutoka asilimia 7.5 katika mwaka wa fedha uliopita.
Iwapo bajeti hiyo itaidhinishwa na bunge, serikali itatumia shilingi bilioni 146 kwa miradi ya urithi wa Kenyatta chini ya kile kinachojulikana kama Ajenda Nne Kuu, ambayo inaangazia usalama wa chakula, nyumba za bei nafuu, huduma za afya za bei nafuu na utengenezaji.
Ni bajeti ya mwisho kabla ya Kenyatta — ambaye ana hudumu mihula miwili pekee kama rais chini ya katiba – atakuwa anaondoka madarakani baada ya takriban muongo mmoja.
Serikali pia inapanga kutumia mabilioni ya dola katika miradi ya miundombinu kama vile barabara kuu inayolenga kurahisisha barabara zenye msongamano wa magari katika jiji kuu la Nairobi na upanuzi wa mtandao wa reli wa taifa ambao haujatunzwa vizuri.
Kulingana na takwimu za Benki Kuu ya Kenya, deni la umma lilifikia shilingi trilioni 8.2 mwezi Desemba.
Uchina ni mkopeshaji wa pili kwa ukubwa nchini Kenya baada ya Benki ya Dunia na imefadhili miradi kadhaa ya miundombinu ya gharama kubwa ambayo imezua wasiwasi kuhusu Nairobi kuchukua deni zaidi kuliko uwezo wake.
Bajeti hiyo pia inaeleza mipango ya kutenga shilingi bilioni 21.7 kwa halmashauri ya uchaguzi ili kuandaa uchaguzi wa rais na wabunge wa Agosti 9, pamoja na shilingi bilioni 22.9 ambazo tayari zishatolewa.
Yatani alisema alipanga kupunguza ushuru kwa bidhaa za petroli, ambayo itakauwa afueni katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na uhaba mkubwa wa mafuta.
Matangazo ya pombe na kamari hata hivyo yatavutia ushuru wa ziada wa asilimia 15, alisema.