Raia 60 wa Zimbabwe wameuawa na tembo kufikia sasa mwaka huu, kwani mafanikio ya uhifadhi yamesababisha kuongezeka kwa migogoro na binadamu, msemaji wa serikali alisema Jumanne.
Zimbabwe inashikilia nafasi ya pili kwa idadi kubwa ya tembo duniani ikiwa na tembo 100,000 baada ya Botswana, na takriban robo moja ya ndovu katika barani Afrika.
Tofauti na sehemu kubwa ya dunia, ambako wawindaji haramu wameua wanyama hao kwa ajili ya pembe zao, idadi ya tembo nchini Zimbabwe inaongezeka kwa takriban asilimia tano kwa mwaka.
“Katika baadhi ya maeneo, tembo wanatembea katika makundi mengi na wamekula kila kitu mashambani na sasa wanahamia kwa makazi ya watu na kuwalazimu waakazi kulipiza kisasi,” msemaji wa serikali Nick Mangwana alisema kwenye Twitter.
“Tembo Waliojeruhiwa wamekuwa wakali na wasioweza kudhibitiwa,” Mangwana alisema.
“Suala la migogoro ya binadamu na wanyamapori limekuwa la kusisimua sana. Mwaka huu pekee Wazimbabwe 60 wamepoteza maisha kutokana na tembo huku wengine 50 kujeruhiwa,” alisema.
Mangwana alisema tembo waliua watu 72 mwaka wa 2021. Tembo wamekuwa wakirandaranda nje ya mbuga za wanyama Zimbabwe.
Lakini ongezeko la idadi ya watu pamoja na umaskini umewalazimu wakazi wa vijijini nchini Zimbabwe kuhamia katika maeneo ambayo yanawaweka katika migogoro na tembo.
Zimbabwe ina idadi ya watu karibu milioni 15 ambayo inakua kwa karibu asilimia 1.5 kwa mwaka.
Tinashe Farawo, wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mbuga na Wanyamapori ya Zimbabwe, aliiambia AFP alionya kuhusu maafa iwapo idadi ya tembo haitapunguzwa.
“Tishio hilo huenda likaongezeka tunapoelekea msimu wa kiangazi ambapo wanyama hao wataenda kutafuta maji na chakula,” alisema.
Farawo alisema wahudumu wa wanyama pori wametumwa kuwauawa tembo hatari zaidi.
Wahifadhi wanasema kuwa Zimbabwe inauwezo wa kuwa na takriban tembo 45,000 pekee, na wanahitaji maeneo makubwa ya malisho.
Biashara ya tembo imepigwa marufuku kimataifa, lakini serikali imeanza kuzingatia leseni za mpango wa uzazi kwa tembo hao au uwindaji ili kukabiliana na ongezeko la wanyama hao.